Mnasumbuka nini.
We njoo huku ununue gari,halafu unatembelea huku ukichoka unapanda boti unarudi dar.
Kila ukisikia hamya gari yako unakuja tena una drive eeeeeeeeeeee kisha unapanda boati unarudi zako.
Wengie hupenda kununua gari zanzibar sifa moja kuu ni hali ya gari,Dar usanii mwingi sana kwenye hizi Yards tofauti na Zanzibar.
Hakuna cheating za kipumbafu kwenye magari,mtu anakuuzia kutokana na uhalisia wake,ndio maana watu wengi na hata jioni ukienda pale Sands Port unakuta gari kibao zinasafirishwa.Na pia watu wengi binafsi wanatumia gari kwa muda mfupi kisha anauza kwa bei alionunulia na sio kibiashara.
Na ndio maana sie tuliopo huku ukitaka gari hata yard huendi,unaenda kuitoa ndani ya uwa wa Mtu.Unless hali iwe ngum kutokana na aina ya gari.
Bado Zanzibar ni bora Zaidi kwa watu kuja kununua Magari,suala la kodi ni suala la kawaida,hizi ni nchi mbili tofauti.
Sio kuweka kigezo cha muungano basi kila kitu kijiendee tu,mbona Kenya imo ndani ya muungano wa Africa Mashariki na walizuia gari za Tanzania kubeba watalii Kenya.Hata elim ya Darasa la tatu inatosha kujua hili suala la Maslahi ya Kiuchumi kwa nchi husika.