Gharama za Lipa kwa simu mbona zimepanda sana?

Gharama za Lipa kwa simu mbona zimepanda sana?

CCM hawanaga akili. Hilo ndilo jibu. Wameona mapato kwenye mobile money transactions yameshuka sasa wamehamia kwenye lipa namba ili wakamate mapato huko.

Majitu majinga kuwahi kutokea serikalini. Hivi wakati dunia inapambana kutoka kwenye physical cash na kuhamia kwenye digital transactions yenyewe yapo busy ku discourage hio mode of transaction.
 
Kudadeki; mimi nina line ya lipa leo nimetoa laki 495,000/= kwa Wakala wamenichinja 3500 ambapo awali ilikuwa ni free kutoa mara1 kwa siku, hizi Lipa Namba sasa ni rasmi zimekosa maana
 
Leo nilikuwa natumia huduma ya Lipa kwa simu kupitia voda, nikalipia bidhaa yenye thamani ya elfu 15 nikakatwa sh. 850, kama sijasahau hii huduma hapo mwanzo ilikuwa na lengo la kumsaidia mteja pale anapolipia bidhaa, ilianza kwa mteja kulipia bidhaa bila kukatwa, then wakaja na makato madogo, sahivi yamezidi kuwa makubwa.

Kwa mwendo huu hii Lipa itakuwa na msaada kweli uliokusudiwa ama ndio wameona dili lipo huku baada ya kubanwa na serikali kwenye M-Pesa kwa makato lukuki? Sijajua kwa mitandao mingine, ila nafikiri kama Voda 'mtandao mama' wamepandisha basi na mitandao mingine itapandisha. Cc vodacom

Yaani ni Upuuzi sana huu wa lipa kwa simu ,ilitakiwa iwe Free maana unalipia bidhaa instead ya cash ,Je wale wanaoswap card sumpermarket wanakatwa malipo ya ziada?
 
Moja ya rafiki zangu wa karibu anafanya biashara hii. Anadai kuwa
"Katika kitu cha kipuuzi katika biashara hii ni kumuunga mteja kifurushi. You may find una wateja watano wote wanasubiri waungwe eti Dk za Jero, mara MBs "
Indeed
 
1100 kwa muamala mmoja ni faida nzur mbona ... mawakal wakubwa kwa siku anaweza fanya hata miamala 100 ya design hiyo so kwa siku akapata 110000

Mkuu unatakaje zaid ya hapo
Utoe 300000 upewe 1100 sio 550 kama sio 600
 
Vitu vingi vimepanda bei kiujumla sasa maisha ni ghali sana
 
Back
Top Bottom