Gharama za ujenzi TZS 13M

Gharama za ujenzi TZS 13M

Albizo

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
284
Reaction score
208
Wakuu habari,

Muda siomrefu natarajia kuanza ujenzi maeneo ya kigamboni. Ramani nilishapata hadi kibali sasa imebaki mimi tuu kuanza. Kuna fundi mmoja nilimtafuta anikadirie gharama na gharama za material tulizo kadiria kuanzia msingi hadi lenter zilikuja TZS 9.6M na yeye akasema ya ufundi itakuwa 2.5M hadi hapo kwenye lenter.

Sasa waungwana naombeni ushauri wenu kama gharama ni reasonable. Nyumba ni vyumba3 ukubwa wa sqm 150 hv. Fundi ni mzoefu.

Nawasilisha.
 
Hivi ukimaliza kuweka Gyspum, nini kinafuata tiles? au skimming? naomba ushauri kwa wazoefu...
 
Tiles ni kitu cha mwisho kabla ya rangi
Kwa hiyo baada ya kumaliza Gypsum, kuvuta wire za umeme, nini kinafuata, kati ya tiles na kumalizia vifaa vya bomba masinki?
 
Sio fundi Maiko kweli huyo-joking
Fundi Maiko wa kijijini wana nyoosha vizuri na bei zao poa sana. Vijijini kwasababu ya kutokua na iuhakika wa maji vyoo ni vya nje na jiko halina sink. Ni mwendo wa sebule dining na vyumba vya kulala.

Uzuri wake mwenye jengo kijijini unaweza kuwa ni wewe peke yako, kama vifaa vyote unavyo ni wiki mbili tu nyumba una paua.
 
Wakuu habari,

Muda siomrefu natarajia kuanza ujenzi maeneo ya kigamboni. Ramani nilishapata hadi kibali sasa imebaki mimi tuu kuanza. Kuna fundi mmoja nilimtafuta anikadirie gharama na gharama za material tulizo kadiria kuanzia msingi hadi lenter zilikuja TZS 9.6M na yeye akasema ya ufundi itakuwa 2.5M hadi hapo kwenye lenter.

Sasa waungwana naombeni ushauri wenu kama gharama ni reasonable. Nyumba ni vyumba3 ukubwa wa sqm 150 hv. Fundi ni mzoefu.

Nawasilisha.
Itatosha, ila bila mchoro utakuwa unafanya kiholela.
 
Wakuu habari,

Muda siomrefu natarajia kuanza ujenzi maeneo ya kigamboni. Ramani nilishapata hadi kibali sasa imebaki mimi tuu kuanza. Kuna fundi mmoja nilimtafuta anikadirie gharama na gharama za material tulizo kadiria kuanzia msingi hadi lenter zilikuja TZS 9.6M na yeye akasema ya ufundi itakuwa 2.5M hadi hapo kwenye lenter.

Sasa waungwana naombeni ushauri wenu kama gharama ni reasonable. Nyumba ni vyumba3 ukubwa wa sqm 150 hv. Fundi ni mzoefu.

Nawasilisha.
Miaka ya nyuma kidogo nilikuwa natafuta nyumba ya kununua. Bei nilizokuwa nakutana nazo zikawa hatoi maana yoyote kwangu, hivyo nikaamua kujenga mwenyewe kwa usimamizi wangu binafsi. Katika hiyo process nikagundua kuwa gharama za ujenzi siyo kubwa za kutisha ila kuna upigaji mwingi sana usipokuwa na usimamizi mzuri. Niliwahi kuleta hapa mchanganuo wa project yangu moja ya vyumba sita ambayo mthamini anaweza kukuambia milioni 100 hadi 150, lakini gharama zangu hazikufika zaidi ya milioni 15 ujenzi wote pamoja na finishing na upakaji rangi. Nilitumia mabati mekundu ya aluminium siyo vigae.

Kwa hiyo kwenye ujenzi, inabidi ukae beneti na fundi hasa upande wa materials. Inaonekana kama vile fundi wako kawa mwungwana kwako kuhusu materials lakini vile vile inategemea na ukubwa wa nyumba yenyewe.
 
Uko sahihi Sana mdau!! Material nunua mwenyewe tu. Yani kila kitu chako
 
Wakuu habari,

Muda siomrefu natarajia kuanza ujenzi maeneo ya kigamboni. Ramani nilishapata hadi kibali sasa imebaki mimi tuu kuanza. Kuna fundi mmoja nilimtafuta anikadirie gharama na gharama za material tulizo kadiria kuanzia msingi hadi lenter zilikuja TZS 9.6M na yeye akasema ya ufundi itakuwa 2.5M hadi hapo kwenye lenter.

Sasa waungwana naombeni ushauri wenu kama gharama ni reasonable. Nyumba ni vyumba3 ukubwa wa sqm 150 hv. Fundi ni mzoefu.

Nawasilisha.
Mkuu, nafikiri nenda kwa aliyekuchorea msikilize ushauri wake ili upate kilichobora.....

Ili kupata ubora nafikiri mtafute architects kama anayonafasi asimamie hiyo kazi kwa kumsimamia fundi au aje na fundi wake......
 
Wakuu habari,

Muda siomrefu natarajia kuanza ujenzi maeneo ya kigamboni. Ramani nilishapata hadi kibali sasa imebaki mimi tuu kuanza. Kuna fundi mmoja nilimtafuta anikadirie gharama na gharama za material tulizo kadiria kuanzia msingi hadi lenter zilikuja TZS 9.6M na yeye akasema ya ufundi itakuwa 2.5M hadi hapo kwenye lenter.

Sasa waungwana naombeni ushauri wenu kama gharama ni reasonable. Nyumba ni vyumba3 ukubwa wa sqm 150 hv. Fundi ni mzoefu.

Nawasilisha.
Hongera sana kwa maandalizi ya ujenzi, kwa uzoefu wangu hiyo pesa itakusogeza lakini haiwezi kumaliza. Msingi na kupandisha Boma Kwa 2.5m ni fair sana.
 
Back
Top Bottom