Gharama za ujenzi TZS 13M

Huu ni ujenzi wa style ipi? Vifaa ulitumia ya aina gani ndugu make mabati na mbao tu kabla ya ufundi inakimbiza 9milioni
 
Huu ni ujenzi wa style ipi? Vifaa ulitumia ya aina gani ndugu make mabati na mbao tu kabla ya ufundi inakimbiza 9milioni
SHapa ndipo ninaposema thamani za nyumba kwetu zinakuzwa kuliko uhalisi, na inawezekana kwa vile tunachukulia nyumba kuwa sehemu ya utajiri wakati nyumba ni hitaji la kawaida la kila binadamu. Ingawa sina namba kamili ya pesa nilizotumia kwenye ujenzi huo, ila ulikuwa ni kidogo sana. Ninakumbukua tunilitumia matofari ya kuchoma sikumbuki kiasi gani, sementi pia sikumbuki mifuko mingapi na bei ya wakati huo; ni kipindi kifupi sana kabla bei ya haijapanda jambo lililofanya waziri mkuu aingile kati na mafundi waliniambia nilipata bahati sana ya kununua mifuko mingi mapema. Mabati mekundu ya aluminium wao wakiyaita ya South ambayo pia sikumbuki idadi yake sasa, na vioo tinted ambayo sikumbuki ni mapande mangapi. Tulitumia rangi za aina nne tu kwa nyumba yote, ila idadi yote ya ndoo zote pia siikumbuki tena; hatujakamilisha uwekaji wa vigae kwenye floor kwani sikupenda vigae vilivyokuwapo madukani wakati huo, na sasa hivi kila ninaporudi nyumbani hukuta kuna watu wanaishi ndani ya nyumba hiyo. In general gharama ilikuwa ni ndogo sana kuliko makadirio yaliyotolewa na wataalamu baada ya nyumba kuisha. Ukitaka kufuatilia endelea kunitag katika topic hii nitaweza kufumua financial record zangu kukupa namba kamili za ujenzi huo.
 
kwa gharama za vifaa vya ujenzi zilivo juu nahs utaishia levo ya madirisha
 
Kwa hiyo baada ya kumaliza Gypsum, kuvuta wire za umeme, nini kinafuata, kati ya tiles na kumalizia vifaa vya bomba masinki?
Wire za umeme
Gypsum
Skimming
Tiles
Rangi
Masinki / switches na taa
 
Mkuu Mimi ni mtu wa site tokea 2013 nilipomaliza chuo kikuu, Nina Jenga nyumba yangu ya tatu Sasa...muda wote huo nimekua nikisimamia ujenzi mwenyewe lakini sijawahi kuona gharama ndogo kiasi hicho.
 
Kwa hiyo baada ya kumaliza Gypsum, kuvuta wire za umeme, nini kinafuata, kati ya tiles na kumalizia vifaa vya bomba masinki?
1:skimming
2:tiles
3;msasa
4:rangi
5: switch + vifaa vya bomba
NB: hakikisha unabakisha rangi ya kidogo ili kabla ya kuhamia unafukia michubuko
 
Mkuu Mimi ni mtu wa site tokea 2013 nilipomaliza chuo kikuu, Nina Jenga nyumba yangu ya tatu Sasa...muda wote huo nimekua nikisimamia ujenzi mwenyewe lakini sijawahi kuona gharama ndogo kiasi hicho.
In fact wakati ninajenga, niliamua kusimamisha nyumba tatu kwa mpigo, mbili zilikuwa ndogo za vyumba vitatu vitatu, lakini hiyo ya tatu ambayo ndiyo ilikuwa lengo langu ilikuwa ni kubwa ya vyumba sita, vyoo vitatu, jiko na stoo. Ni kutokana na gharama kuwa kidogo ndiyo maana nilifanya hivyo na mpaka sasa hivi ninavyoandika kuna matofari ya kutosha nyumba moja bado yako pale nyumbani kwani hayakuisha. Nitakuwapo tena mwezi wa sita mwaka huu kwa muda mrefu kidogo kama Covid haitavuruga tena kama ilivyotokea miaka miwili iliyopita. Nitakuarifu ni project gani nyingine tutafanya.
 
Hivi ukimaliza kuweka Gyspum, nini kinafuata tiles? au skimming? naomba ushauri kwa wazoefu...
Skim kwanza na maliza shughuli za juu kisha ndo uanze na Tiles chini.Hii inaokoa kuvunja tiles kwa kuweka ngazi n.k juu yake wakati wa kuskim/rangi.
 
Mkuu...Kwa kutokuwa na kumbukumbu ya vitu vingi hivi vya muhimu katika ijenzi..unawezaje kukumbuka jumla ya gharama ??

Naomba niwe wa mwisho kuamini hili..
 
Mkuu...Kwa kutokuwa na kumbukumbu ya vitu vingi hivi vya muhimu katika ijenzi..unawezaje kukumbuka jumla ya gharama ??

Naomba niwe wa mwisho kuamini hili..

Ukishaamini unishtue nami nione kama nitafikiria kuamini au lah.!
 
Hivi ukimaliza kuweka Gyspum, nini kinafuata tiles? au skimming? naomba ushauri kwa wazoefu...
Kwa mm fundi rangi uzoefu wangu kinacho fuata skimming kisha tiles alafu rangi unamalizia Aluminium
 
Hiyo bei iko sawa kabisa.
 
Una uhakika na hizo sqm 150?
 
Saa nyingine kuna kudanganyana humu JF. Eti M15 inamaliza nyumba ya vyumba 3. Jamani hii kweli au? Mie siamini kabisa. Anyways, kuna nyumba na vijumba pengine. Kuna vijumba nimeingia unakuta jikoni space ni kama stoo. Inabidi hata kupika wanapikia nje kupata nafasi. Na ukubwa wa vyumba vya kulala ukiweka kitanda tu vimejaa. Hakuna nafasi hata kidogo. Pengine nyumba kama hizo labda inaweza kuwa zimecost M15. Ila kwa nyumba nzuri ya nyumba vitatu yenye nafasi na finishing ya kupendeza, sidhani kama itapungua Million 50. Na pengine ikawa zaidi ya hapo. Nimesoma comment hapo juu kuna mmoja kasema kajenga nyumba ya vyumba sita na mambo mengine kwa M15. Labda ilikuwa miaka ya nyuma sana na inawezekana pia maeneo ya kijijini? Hapo inawezekana. Ila kwa maisha haya ya sasa, sidhani kama M15 itakamilisha. Ila sijui. Watu tunatofoutiana katika kukadiria na uhalisia.
 
Nyumba ya mil 50 ni nyumba yenye mbwembwe nyingi zisizo na ulazima. Nyumba ya kawaida ya vyumba 3 ukiwa na mil 27-30 unajenga
 
Ukifika kwenye Tiles nicheki nikupe tiles kwa bei poa..
0744928908
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…