SHapa ndipo ninaposema thamani za nyumba kwetu zinakuzwa kuliko uhalisi, na inawezekana kwa vile tunachukulia nyumba kuwa sehemu ya utajiri wakati nyumba ni hitaji la kawaida la kila binadamu. Ingawa sina namba kamili ya pesa nilizotumia kwenye ujenzi huo, ila ulikuwa ni kidogo sana. Ninakumbukua tunilitumia matofari ya kuchoma sikumbuki kiasi gani, sementi pia sikumbuki mifuko mingapi na bei ya wakati huo; ni kipindi kifupi sana kabla bei ya haijapanda jambo lililofanya waziri mkuu aingile kati na mafundi waliniambia nilipata bahati sana ya kununua mifuko mingi mapema. Mabati mekundu ya aluminium wao wakiyaita ya South ambayo pia sikumbuki idadi yake sasa, na vioo tinted ambayo sikumbuki ni mapande mangapi. Tulitumia rangi za aina nne tu kwa nyumba yote, ila idadi yote ya ndoo zote pia siikumbuki tena; hatujakamilisha uwekaji wa vigae kwenye floor kwani sikupenda vigae vilivyokuwapo madukani wakati huo, na sasa hivi kila ninaporudi nyumbani hukuta kuna watu wanaishi ndani ya nyumba hiyo. In general gharama ilikuwa ni ndogo sana kuliko makadirio yaliyotolewa na wataalamu baada ya nyumba kuisha. Ukitaka kufuatilia endelea kunitag katika topic hii nitaweza kufumua financial record zangu kukupa namba kamili za ujenzi huo.