Gharama za ushuru wa mzigo kwa Cubic meter (CBM) kutoka China

Gharama za ushuru wa mzigo kwa Cubic meter (CBM) kutoka China

Joined
Nov 13, 2011
Posts
36
Reaction score
10
Ndugu wanajamvi kwa wanaofahamu naomba wanijuze,

Ninafikiria kusafiri kwenda uchina kwa lengo la biashara ya nguo. Kabla ya kufanya hivyo ningependa niyajue mambo kadha wa kadha likiwemo hili la gharama za ushuru hapa kwetu TZ, nimepeleleza na kuambiwa ushuru unalipwa kutokana na cubic metre ya mzigo wako, kwa anefahamu tafadhali anifahamishe zaidi.

Pia ningependa kufahamu ni agent gani mwenye gharama nafuu na reliable kwa kusafirisha mizigo kutoka China.

Naomba kuwasilisha mada.
 
Ndugu wanajamvi kwa wanaofahamu naomba wanijuze,
Ninafikiria kusafiri kwenda uchina kwa lengo la biashara ya nguo.Kabla ya kufanya hivyo ningependa niyajue mambo kadha wa kadha likiwemo hili la gharama za ushuru hapa kwetu tz.nimepeleleza na kuambiwa ushuru unalipwa kutokana na cubic metre ya mzigo wako.kwa anefahamu tafadhali anifahamishe zaidi.
Pia ningependa kufahamu ni agent gani mwenye gharama nafuu na reliable kwa kusafirisha mizigo kutoka China.
Naomba kuwasilisha mada.

Bwana Robemongi gharama za bandari na za kutuma mzigo ndio zinaangalia CBM ,Ushuru autazami CBM,wanaangalia kitu kilichomo ndani..uwa napenda sana kuwashauri watu wanaopenda kufanya biashara ya kuingiza bidhaa kama wewe.
Njia nzuri kabisa ambayo naona wakongo na west afrika wanayotumia ni kuungana,faida wanazozipata ni nyingi nilizieleza hapo nyuma lakini naomba nirudie kidogo,moja ya faida ni ticket mkiwa kama watano ni lazima mpate rate nzuri kwenye airline,pili sehemu za kibiashara kama China,Dubai,Thailand nk uwa kuna hoteli maalumu kwa ajiri ya wafanyabiashara kuna vyumba vina twin bed hivyo mna share na cost inakuwa chini zaidi,tatu ni kwenye kununua mzigo hapo ndio kwenye umuhimu mkubwa maana mkiwa at least watano mtanunua mzigo mkubwa hivyo price itakuwa chini wenyewe wanasema FACTORY PRICE...Nne mkiwa wengi hautatuma mzigo kwa kupima CBM,unajua shipping agent uwa wananunua nafasi ya container kwenye meli,mfano container ya ft 20 toka Dubai-Tz ni $1700 kisha wanasubiri watu wenye mizigo midogodogo na wanakucharge kwa nafasi CBM ukipiga hesabu utakuta yeye anapata zaidi ya $3500,sasa kama mpo at least watano mtakodisha container zima ambalo mtachanga pesa kidogo sana,mwisho mkishatuma mzigo wenu mta CLEAR bandarini kama container hapo pia mtachangia pesa kidogokidogo.Wafanyabiashara pale Kariakoo wanafanya hivyo ndio maana ukienda kwenye maduka ya nguo au ya vifaa vya umeme bidhaa zao zinafanana sana maana wengi wao wanachukua mzigo sehemu moja.Wewe kama wewe unawezafanikiwa kama ukishapata uzoefu,lakini TWO HEADS ARE BETTER THAN ONE...all the best.
 
Thanks kwa ufafanuzi luck saba saba,ntaendelea na research zaid,ili niweze kujipanga vyema kwa wazo langu.
 
HSC ndiyo mkombozi wako, wanakupa bei ya nauli pamoja na kodi bandarini unapokea mzigo ukiwa cleared unaenda kuuza tu!
 
HSC ndiyo mkombozi wako, wanakupa bei ya nauli pamoja na kodi bandarini unapokea mzigo ukiwa cleared unaenda kuuza tu!
Hawa HSC si ndio wale walioleta shida kwa wafanyabiashara wa Kariakoo???ma container yakashikwa na TRA na bosi wao kumwagiwa tindikali???kama ndio hao mambo yao yalishagundulika,sio deal tena
 
Hawa HSC si ndio wale walioleta shida kwa wafanyabiashara wa Kariakoo???ma container yakashikwa na TRA na bosi wao kumwagiwa tindikali???kama ndio hao mambo yao yalishagundulika,sio deal tena

Haohao, mbona bado wanapiga kazi mkuu, si unajua ukila na wakubwa!
 
Back
Top Bottom