Gharama za vifurushi vya intaneti zapandishwa tena kimya kimya. Je, ni censorship ya aina yake?

Gharama za vifurushi vya intaneti zapandishwa tena kimya kimya. Je, ni censorship ya aina yake?

Dr Mwigulu anasemaje? Je, ongezeko linatokana na tozo?
 
Dah hicho kifurushi cha 50,000 kilikuwa kinauzwa 35,000 wamepandisha 15,000 ni nyingi hii itaumiza sana haswa kwa biashara za online

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Bando langu lilikata asubuhi, naangalia ofa yangu nakuta haipo tena...nahamia Burundi kama mwigulu alivyotaka.
 
TTCL hata gharama ya muda wa dakika wamepandisha bei sana.

Eti dakika 100 shilingi 4,000-5,000 ??’!!

Inasikitisha sana
 
Haya ndo mambo tunayotaka...

Kazi iendelee hutaki hamia Burundi.
 
Mie nafaidi tigo post pay 30Gb kwa 25K per month.
 

Ni mwendo ule ule, umafia wa kimya kimya, kwa Voda na Tigo wameanza kutesti mitambo kwa kkupunguza GB za vifurushi vya mwezi.

Kuanzia sasa tutegemee lolote, hii ni trailer tu, bado muvi kamili ya machinjo yatayofanyika kimya kimya gizani usiku wa manane, nadhani tunaweza kuamka asubuhi mabadiliko kadha na kadha yakiwa yamefanyika kwenye vifurushi vingine.

Mapato ndio issue
 
Back
Top Bottom