Gharama zinazoambatana na serikali tatu, mpo tayari kodi zipande?

Gharama zinazoambatana na serikali tatu, mpo tayari kodi zipande?

Mimi nadhani pendekezo la tume la serikali tatu ni improved objectives au malengo la EAC. Rotation ya kiti, michango ya areas za muungano inakaribiana na yale yale ya EAC na EU.
Je nchi (ie Zanzibar au Tanzania bara) isipochangia kikamilifu, nini kitafuata?
Kuwa na mapendokezo haya ni sawa lakini kama mojawapo ya sehemu ya muungano isipotimiza wajibu wake , ni nini kita fuata. Zanzabar inashindwa kulipia matumizi yake ya umeme Tanesco kwa sasa.
Wilaya za Ilala, Kinodoni na Temeke individually zinaishinda Zanzibar kwa mapato.
 
warioba kakiri kuwa gharama zitaongezeka lakini itungwe sheria ili kusimamia mapato na matumizi na namna jisni serilai itakavyoendeshwa kwa kuepuka gharama, hii ni ajabu kabisa kuwapa wanachi gharama mara mbili zaidi kwa lengo la kufurahishana
 
Mbona mikoa na wilalaya zinavyoongezwa hamhoji kuwa gharama za uendeshaji zinaongezeka au kwa kuwa zinawafaidisha wanasiasa.

Hapa jibu ni serikalI tatu na uendeshaji tunachangia 50/50 na Zanzibar, hamna cha kusema inchi ndogo wala uchumi mdogo. kama ni gharama kwetu na Zanzibar pia ni gharama.

CCM acheni kuturubuni, hapa tulipo tu kodi zimejaa kila idara. na hazitusaidii chochote zaidi ya kuongeza deni la Taifa.

Kama haiwezekani serikali tatu moja ndio suluhisho.!
...............au kila mtu ajue lake
 
Watanzania hatushtushwi na ongezeko la kodi. Pandisha umeme, poa tu, pandisha bei za bidhaa madukani, nauli za mabasi, ada za shule... poa tu. Njoo Tanganyika yetu tupo tayari hata kula majani kama tulivyofanya ili Nkapa apate pipa la kutalii.
 
SMU kinachofanyika ni zaidi ya kutofautisha gharama na mapato kati ya Tanganyika na Zanzibar, pia wanaongeza serikali mpya ya Tanganyika na hiyo ni gharama mpya.

Aidha unapotosha makusudi ama hujui unacho kijadili. Wizara zote ambazo sasa hivi kazi zake siza Muungano zitarudishwa Tanganyika! Serikali ya Zanzibar tayari ipo! Wizara zinazohusika na Muungano zitaunda Serikali ya JMT!

Wizara zote na Taasisi hizi zipo kazi ni kuzipachika chini ya mamlaka husika! Cheo cha Waziri Mkuu wa JMT kinatakiwa kubadilishwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika!

Gharama ambazo CCM inapigia kelele sasa ni unafiki wa hali ya juu kutokana na wingi wa Wizara na Baraza kubwa la Mawaziri wasio na tija! Uanzishaji mikoa kwasababu ya kisiasa badala ya uimarishaji miundombinu,zahanati na utawala bora ngazi zote! Wananchu hawana sababu ya kuonana na Wakuu wa Mikoa n Wilaya kama huduma muhimu zinapatikana na watendaji kuanzia ngazi ya chini wanatekeleza wajibu wao.
 
Its a means to an end... (means) Serikali Tatu (end) Muungano kuvunjika. Sababu watu walikatazwa kuongelea direct kuvunja muungano hii ndio option iliyobaki. Sababu Serikali Moja haiwezekani, Mbili za sasa Tanganyika wanasema wanaonewa so.., what do you suggest ?
 
Warioba na tume yake haijazingatia hilo, wao wameengalia manufaa ki siasa tuu

Misamaa ya kodi na mapesa yanayotoroshwa kwenda nje ya nchi kila kukicha na mali asili zetu tulizo nazo zikidhibitiwa vilivyo hizo serikali 3 ni rahisi sana.
 
Kama umesoma hapo juu mimi ningependa kodi zetu ziwe nafuu na njia pekee ni kuwa na serikali moja kama unavyosema ili tusijikute kama Kenya ambapo makusanyo makubwa ya kipato cha serikali yanaishia kwenye malipo ya wafanyakazi badala ya miradi ya maendeleo.

Hadi sasa tanzania na kenya nani yupo juu kimawndeleo? Wee unataka kutulinganisha na kenya ki maendeleo?
 
warioba kakiri kuwa gharama zitaongezeka lakini itungwe sheria ili kusimamia mapato na matumizi na namna jisni serilai itakavyoendeshwa kwa kuepuka gharama, hii ni ajabu kabisa kuwapa wanachi gharama mara mbili zaidi kwa lengo la kufurahishana

Wizara na Taasisi hizi zote zipo pengine kama unajadili uanzishwaji wa Bunge la Muungano! Na kumbuka Tanganyika itautua mzigo wa kuhidumia Serikali ya JMT,Zanzibar na Bunge kubwa la JMT linalo jumuisha karibu Wabunge 70 toka Zanzibar wanaokuja kushiriki ktk shughuli zisizo wahusu! Sasa tutapeleka Wabunge wachache nadhani 50 kuiwakilisha Tanganyika!

Ndani ya Serikali yetu ya Tanganyika tunaweza kuangalia upya majimbo ya uchaguzi kwa kupunguza na kuondoa viti vya dezo! Muhimu tuimarishe Taasisi za kiutendaji ili zitatue kero za wananchi.
 
The Union of Tanzania is for whom? manake the Tanganyikan people and Zanzibaries don't like it....
 
Wakati tupo busy na mijadala ya Muungano naona ni bora nikumbushe watu kuhusu Bili zitazokuja na uwepo wa serikali tatu ambazo kwa bahati mbaya mimi na wewe ..ndio na wewe (usishangae) itabidi tuchangae kupitia kodi zetu. Kwa akili yangu ya kawaida siamini Rais,Wabunge na watendaji wengine kwenye serikali ya Tanganyika hawatutanga sheria za kodi ambazo zitaniumiza mimi (mwananchi) iliwapate marupurupu yao. Ningependa kupata mawazo tofauti juu ya hili suala. Karibuni.

kasome kwanza rasimu ya pili ya katiba na kama hujui kusoma muombe hata mwanao wa chekechekea akusomee. hiki ulichoandika hapa ni sawa na kujivua nguo mkuu. ukisoma vizuri ile rasimu utatama warioba na wenzake waishi miaka 8000.
 
Wakati tupo busy na mijadala ya Muungano naona ni bora nikumbushe watu kuhusu Bili zitazokuja na uwepo wa serikali tatu ambazo kwa bahati mbaya mimi na wewe ..ndio na wewe (usishangae) itabidi tuchangae kupitia kodi zetu. Kwa akili yangu ya kawaida siamini Rais,Wabunge na watendaji wengine kwenye serikali ya Tanganyika hawatutanga sheria za kodi ambazo zitaniumiza mimi (mwananchi) iliwapate marupurupu yao. Ningependa kupata mawazo tofauti juu ya hili suala. Karibuni.

Links:-

1.) https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ha-serikali-tatu.html?highlight=serikali+tatu

2.) https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-uraia-pacha-mikopo-na-katiba-tanganyika.html
 
Wakati tupo busy na mijadala ya Muungano naona ni bora nikumbushe watu kuhusu Bili zitazokuja na uwepo wa serikali tatu ambazo kwa bahati mbaya mimi na wewe ..ndio na wewe (usishangae) itabidi tuchangae kupitia kodi zetu. Kwa akili yangu ya kawaida siamini Rais,Wabunge na watendaji wengine kwenye serikali ya Tanganyika hawatutanga sheria za kodi ambazo zitaniumiza mimi (mwananchi) iliwapate marupurupu yao. Ningependa kupata mawazo tofauti juu ya hili suala. Karibuni.

Kwa mtazamo wangu wa kimahesabu, serikali moja ua tatu zitakuwa na gharama nafuu zaidi kuliko mbili tulizonazo sasa.
 
Wakati tupo busy na mijadala ya Muungano naona ni bora nikumbushe watu kuhusu Bili zitazokuja na uwepo wa serikali tatu ambazo kwa bahati mbaya mimi na wewe ..ndio na wewe (usishangae) itabidi tuchangae kupitia kodi zetu. Kwa akili yangu ya kawaida siamini Rais,Wabunge na watendaji wengine kwenye serikali ya Tanganyika hawatutanga sheria za kodi ambazo zitaniumiza mimi (mwananchi) iliwapate marupurupu yao. Ningependa kupata mawazo tofauti juu ya hili suala. Karibuni.
Warioba na tume yake haijazingatia hilo, wao wameengalia manufaa ki siasa tuu
Katika watu wajinga ambao sijui hata mmewezaje kuwa wana JF, ninyi WILE na MNAMBOWA kweli mmetia fora. Eti Warioba na tume yake hawajazingatia suala la gharama! Hii mmetoa wapi? Mmeisoma Raismu yote kama ilivyotolewa au mnabwabwaja tu kama mazezeta? Mnapata wapi jeuri ya kuchangia na kuanza kulalama kumbe hata Rasimu yenyewe kama ilivyotolewa na Mh. Jaji Sinde Joseph Warioba hamjaisoma? This is stupidity at its peak and how I hate stupidity! Point za kipuuzi kama hizi heri zipigwe marufuku kwani zinashusha hadhi ya JF.
 
Stupid? I'll tell you something about stupidity, It's stupid kwa mtu kama wewe na Mh. Warioba kwanza kukubali kwamba Wazanzibari hawataki Muungano halafu mnakuja na proposal ya serikali tatu huku mkijua suluhusho ni kwa wazanzibari kupewe uhuru lakini no nyie si mna akili mkaona the best way around it nikutuongezea magharama kupitia serikali tatu, Also its stupid and ignorance ku assume gharama itakuwa sawa na ya saa hizi pale serikali ya tatu ikiongezeka, its simple mathematics hata sijui inakuwaje mtu anayejifanya hapendi stupidity kama wewe hawezi kuona the logic behind that. Pia kumbuka hata huyo Mh. Jaji Sinde alisema gharama itaongezeka japo kidogo ukimuuliza aelezee in detail hiyo kidogo anatoa blah blah tu.
 
Back
Top Bottom