Ghasia Rongai: Hasira Za Wanafunzi Wa MMU Zalipuka Baada ya Madai Ya Kushambuliwa

Ghasia Rongai: Hasira Za Wanafunzi Wa MMU Zalipuka Baada ya Madai Ya Kushambuliwa

Wakaguongo

Member
Joined
Sep 23, 2026
Posts
95
Reaction score
38
Hali ya taharuki imetanda katika mtaa wa Bangladesh slum, Ongata Rongai, baada ya nyumba kadhaa kuripotiwa kuchomwa moto wakati wa maandamano ya wanafunzi wa Multimedia University of Kenya (MMU).

Maandamano hayo yanadaiwa kuanza baada ya mwanafunzi mmoja wa MMU kushambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa majambazi, na kuripotiwa kujeruhiwa vibaya hadi mwanafunzi mmoja kulazwa hospitalini.

Baadhi ya wanafunzi waliingia katika maeneo ya jirani wakilalamikia usalama wao. Hali hiyo ilizidi kuwa mbaya huku nyumba kadhaa zikiripotiwa kuchomwa moto na Magadi Road kuvurugwa, huku Polisi wakifika eneo hilo kutuliza hali.

Kwa sasa, mazingira kamili ya uchomaji huo bado hayajawekwa wazi, na taarifa kuhusu nani hasa alichoma nyumba hizo bado zinahitaji kuthibitishwa rasmi.

LAKINI SWALI KUBWA NI HILI:
Ikiwa kweli wanafunzi wamekuwa wakishambuliwa mara kwa mara katika eneo hilo, kwa nini hali ya usalama imefika hatua ya maandamano na nyumba za wakazi kuchomwa? Na zaidi, Je usalama wa wanafunzi unaweza kudaiwa bila kugeuza wakazi wa eneo hilo kuwa waathirika wa hasira?
 

Attachments

  • 1167.mp4
    6.4 MB
Back
Top Bottom