Habari za Zanzibar
JF-Expert Member
- Dec 18, 2024
- 651
- 433
GHATI CHOMETE AUNGANA NA WAOMBOLEZAJI KATIKA IBADA YA KUAGA MWILI WA MHE. LUKUVI, BUNGENI DODOMA
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Mhe. Ghati Zephania Chomete, tarehe 27 Machi 2026 ameungana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb), pamoja na wabunge, viongozi mbalimbali na waombolezaji katika ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Ismani, Marehemu Mhe. William Vangimembe Lukuvi.
Ibada hiyo ya kuaga mwili wa Marehemu Mhe. Lukuvi, aliyefariki dunia tarehe 25 Machi 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma, imeongozwa na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Paulo wa Msalama, Jimbo Kuu la Dodoma, Padri Simon Mswaga, katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.