Wick
JF-Expert Member
- Dec 19, 2012
- 8,313
- 12,170
Umewahi sikia kisa fulani cha 50 Cents kufungiwa kurecord nyimbo yoyote New york City?. Hebu chukulia mfano leo Ney wa mitego ajilipue atunge nyimbo awaimbe wauza madawa wote bongo halafu na wao kumkomoa wanazuia hakuna mtu yeyote Bongo kumrecordia Ney nyimbo.
Basi hiyo ndio ilimtokea 50 cent baada ya kuimba nyimbo fulani akaiita Ghetto Qur'an. Hiyo nyimbo ilivuja miaka ya 2000, yani humo ndani jamaa kawachana wauza madawa wote waliokuwa wanafanya biashara huko South Jamaica, Queens Marekani.
Wafanyabiashara kama Hamsini hivi jamaa aliwasnitch ndani ya nyimbo yake kama Kenneth 'SuPreme' McGriff na binamu yake Gerald Prince Miller hawa wote walikuwa vioongozi wa kundi moja matata la Supreme Team.
Baada ya jamaa kumblacklist 50 Cent studio zote za New York, kuna producer mmoja aliitwa Jam Master Jay yeye akaweka ngumu akaamua kumsaidia 50 Cent kurecord nyimbo kumbuka hapo bado 50 Cent sio huyo tunayemjua leo yani kajamaa ni kaunderground tu halafu kakaamuua kujilipua kurecord kitu ambacho hata wakubwa kama Jah rule walikua hawawezi kukiimba.
Sasa jamaa baada ya kuona kumbe biti lao halijawaingia baadhi ya vinega ikabidi wafanye street justice, 50 Cent akala mvua ya risasi 9 na huyo producer wake akauliwa kwa risasi pia!. Bahati nzuri 50 Cent akapona majeraha lakini ujumbe akawa kapata, akagoma wapa ushirikiano polisi kukamata wabaya wake na ikabidi nyimbo nyingine akazirecord Canada.
Ile nyimbo baadae ilikuja rudia wekwa kwenye mixtape ya 50 Cent ya mwaka 2002 iliyoitwa Guess Who's Back? hivyo ikaendelea itwa jina lake hivyo hivyo "Ghetto Qua'ran".
Huyu Kenneth McGriff ambaye ndio alikuwa kiongozi wa hilo kundi la supreme team alikuja kamatwa na kafungwa kifungo cha maisha bila uwezekano wa kuja samehewa na ni rafiki mkubwa wa Irving au "Irv Gotti" ambaye ndio muanzilishi wa Murder Inc.. Ukitaka kumjua huyo Kenneth "Supreme" McGriff na binamu yake Gerald "Prince" Miller wacheki kwenye movie ya 50 Cent - Get Rich or Die Tryin' wameigizwa kama Levar na Majestic.
Hilo kundi la Supreme Team unaambiwa lilikuwa hatari inakadiriwa lilikuwa na wanachama hadi 2,000 New york City, na mawasiliano yao walikuwa wanatumia code na namba zao maalum hakuna kutumia maneno kikawaida.
Maboss wake walikuwa na mabodyguard kibao halafu wakitaka kwenda sehemu kinatumwa kikosi kinakuwa na radio call watu wanawekwa hadi juu ya maghorofa kuangalia usalama.