Ghetto Qura'n na kisa cha 50 Cent kupigwa risasi..

Ghetto Qura'n na kisa cha 50 Cent kupigwa risasi..

Wick

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
8,313
Reaction score
12,170
Umewahi sikia kisa fulani cha 50 Cents kufungiwa kurecord nyimbo yoyote New york City?. Hebu chukulia mfano leo Ney wa mitego ajilipue atunge nyimbo awaimbe wauza madawa wote bongo halafu na wao kumkomoa wanazuia hakuna mtu yeyote Bongo kumrecordia Ney nyimbo.

Basi hiyo ndio ilimtokea 50 cent baada ya kuimba nyimbo fulani akaiita Ghetto Qur'an. Hiyo nyimbo ilivuja miaka ya 2000, yani humo ndani jamaa kawachana wauza madawa wote waliokuwa wanafanya biashara huko South Jamaica, Queens Marekani.

Wafanyabiashara kama Hamsini hivi jamaa aliwasnitch ndani ya nyimbo yake kama Kenneth 'SuPreme' McGriff na binamu yake Gerald Prince Miller hawa wote walikuwa vioongozi wa kundi moja matata la Supreme Team.

Baada ya jamaa kumblacklist 50 Cent studio zote za New York, kuna producer mmoja aliitwa Jam Master Jay yeye akaweka ngumu akaamua kumsaidia 50 Cent kurecord nyimbo kumbuka hapo bado 50 Cent sio huyo tunayemjua leo yani kajamaa ni kaunderground tu halafu kakaamuua kujilipua kurecord kitu ambacho hata wakubwa kama Jah rule walikua hawawezi kukiimba.

Sasa jamaa baada ya kuona kumbe biti lao halijawaingia baadhi ya vinega ikabidi wafanye street justice, 50 Cent akala mvua ya risasi 9 na huyo producer wake akauliwa kwa risasi pia!. Bahati nzuri 50 Cent akapona majeraha lakini ujumbe akawa kapata, akagoma wapa ushirikiano polisi kukamata wabaya wake na ikabidi nyimbo nyingine akazirecord Canada.

Ile nyimbo baadae ilikuja rudia wekwa kwenye mixtape ya 50 Cent ya mwaka 2002 iliyoitwa Guess Who's Back? hivyo ikaendelea itwa jina lake hivyo hivyo "Ghetto Qua'ran".

Huyu Kenneth McGriff ambaye ndio alikuwa kiongozi wa hilo kundi la supreme team alikuja kamatwa na kafungwa kifungo cha maisha bila uwezekano wa kuja samehewa na ni rafiki mkubwa wa Irving au "Irv Gotti" ambaye ndio muanzilishi wa Murder Inc.. Ukitaka kumjua huyo Kenneth "Supreme" McGriff na binamu yake Gerald "Prince" Miller wacheki kwenye movie ya 50 Cent - Get Rich or Die Tryin' wameigizwa kama Levar na Majestic.

Hilo kundi la Supreme Team unaambiwa lilikuwa hatari inakadiriwa lilikuwa na wanachama hadi 2,000 New york City, na mawasiliano yao walikuwa wanatumia code na namba zao maalum hakuna kutumia maneno kikawaida.

Maboss wake walikuwa na mabodyguard kibao halafu wakitaka kwenda sehemu kinatumwa kikosi kinakuwa na radio call watu wanawekwa hadi juu ya maghorofa kuangalia usalama.
 

Attachments

Duuuuhhhhh,noma sana...huwa kuna movie fulani ya 50 Cent siifaham kwa jina lkn ndani yake huwa kuna mauaji sana na matumizi ya madawa wa kulevya,kama unaifaham kwa jina naomba unifahamishe!
 
Fifty kumbe naee ni mhuni toka ktamboo
50 Cent toka mtoto baada ya mama yake kuuliwa akaenda ishi na wajomba zake unaambiwa jamaa alikuwa anawasupply home mzigo wa cocaine!... Yani mjomba na ndugu wakipata arosto anawaambia kuna rafiki yangu anauza mzigo wanampa hela akawaletee kumbe anazunguka mtaani anarudi anawapa mzigo toka ndani ya nyumba humo humo[emoji2]. Badae alikuja kamatwa na gun shuleni kwao ndio ikabidi awaambie na home yeye ndio supplier wao na anauza sana!!... Jamaa ni gangstar hasa!.
 
Duuuuhhhhh,noma sana...huwa kuna movie fulani ya 50 Cent siifaham kwa jina lkn ndani yake huwa kuna mauaji sana na matumizi ya madawa wa kulevya,kama unaifaham kwa jina naomba unifahamishe!
get rich or die tryin nazanii si humo ndani anarap!?...au street of bloods?
 
50 ni real gangster.. Licha ya kuuza madawa kwa miaka kibao hajui ladha ya cocaine wala heroine.. Hajawahi kuonja. Na alikuwa na adabu sana mbele ya bibi yake hivyo bibi akuwahi kuamini kama mjukuu wake ni jiwe na alianza kulipa bills za Nyumba ya bibi yake akiwa bado mtoto anauza unga street.

Hadi Leo bibi yake 50 anasema 50 ni mpole na mkarimu ila kitaani wanakwambia jamaa ana kauli mbiu yake moja kwamba "show no love..love will get you killed" kwa hiyo yeye kabla hujamkill anakukill wewe.
 
Yap ni kweli, Kenneth Mc Griff yupo jela mpaka Leo,Wise Mc Griff naye yupo jela naye,juzi amemtukana sana 50,Supreme team wamefilisika,Murder inc nayo haina sauti tena,50 ni gangsta for real,niliwahi kukutana naye Houston Niga hana noma kabisa,Lorenzo Fat cat naye hana noma,Mc Griff ndiye aliyemuua Jam Master Jay wa Run DMC,pia Kenneth Mc Griff amemtomba sana mama ake fifty,mama ake fifty naye alikuwa drug dealer,na ukweli ni kwamba Mc Griff ndiye baba mzazi wa fifty,hata nyimbo ya Ghetto Quran ilikuwa Kali,juzi pia 50 ametoa ngoma nyingine kumtukana Mc Griff
 
50 ni real gangster.. Licha ya kuuza madawa kwa miaka kibao hajui ladha ya cocaine wala heroine.. Hajawahi kuonja. Na alikuwa na adabu sana mbele ya bibi yake hivyo bibi akuwahi kuamini kama mjukuu wake ni jiwe na alianza kulipa bills za Nyumba ya bibi yake akiwa bado mtoto anauza unga street.

Hadi Leo bibi yake 50 anasema 50 ni mpole na mkarimu ila kitaani wanakwambia jamaa ana kauli mbiu yake moja kwamba "show no love..love will get you killed" kwa hiyo yeye kabla hujamkill anakukill wewe.
hyo slogan co poa
 
Back
Top Bottom