Traxtion
JF-Expert Member
- Dec 10, 2021
- 8,000
- 16,414
Watu kadhaa wanahofiwa kufunikwa na vifusi wa jengo la ghorofa 13 ambalo limeporomoka katika eneo la Eastleigh Kaunti ya Nairobi nchini Kenya.
Maafisa wa uokoaji wako eneo la tukio wakiendelea na zoezi la kupekua vifusi vya jengo hilo ambalo limeanguka na mpaka sasa majeruhi mmoja amekimbizwa hospitali.
Kwa mujibu wa mashuhuda jengo hilo lilikuwa limekamika sehemu ya chini na palikuwa na maduka ya biashara
Maafisa wa polisi walifika katika eneo la tukio na wanaripotiwa kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya wananchi waliokuwa wamekusanyika, ili kuwawezesha waokoaji kufika kwenye vifusi na kuendelea na shughuli za uokoaji.