Lole Gwakisa
JF-Expert Member
- Nov 5, 2008
- 4,768
- 2,361
MODS mmeondoa thread hiyo hapo juu, ambayo kuna member aliulizia.
Nampa ukweli wa Gibbons Mwaikambo kwa ufupi.
Hii mada hata leo ina somo kubwa.
Watoto waliozaliwa majuzi hawawezi kumfahamu.
Gibbons Mwaikambo alizaliwa 1938 huko Tukuyu, Mbeya na alisomea Economics mpaka kiwango cha shahada ya Masters huko Moscow ,Urusi, 1967.
Gibbons alioana na Ester Mariki, binti wa kichagga.
Baada ya mashirika mengi kutaifishwa Gibbons alikuwa General Manager wa muda mrefu NIC, National Insurance Corporation.
Alisifika kwa kulipaisha kiuchumi shirika hilo na kufikia kuwa shirika moja lenye nguvu kiuchumi.
Baada ya kustaafu, miaka ya 80 akaona ajaribu mkono wake katika siasa.
Awali alikuwa kama sikosei, aidha wadhamini wa chama au idara ya chama ,WAZAZI, hili sina uhakika, lakini alikuwa kiongozi CCM.
Hata hivyo kwa sababu zisizojulikana alifanyiwa ile kitu inaitwa figisu na jina lake katika changuzi za ndani ya CCM halikupitishwa.
Mgombea mwenza wa nafasi hiyo alikuwa Emmanuel Mwabulukutu, afisa aliyekuwa wa muda mrefu wa Idara ya Usalama.
Kuiona hiyo figisu, na kwamba alikuwa kiongozi ndani ya CCM, kwa ghadhabu Gibbons alitaka kufanya maamuzi magumu kujitoa ndani ya chama na kujiunga na TLP, chama chenye nguvu, kilichokuwa cha upinzani kikiongozwa na Lyatonga Mrema.
Siri hiyo aliwaambia rafiki zake wa karibu.
Kosa kubwa.
Hakuna siri ya watu wawili. Na miaka ya Mwalimu kila mtu alikuwa anamchunguza mwenziwe.
Muda si mrefu siri iliwafikia wana Usalama kuwa kesho yake Gibbons anajitoa CCM.
Usiku huo huo Gibbons alitekwa.
Asubuhi yake gari lake lilikutwa limegonga ukuta wa nyumba moja ya kibalozi pale Upanga, naye amekufa ndani yake.
Ni wazi ilikuwa assasination.