monde arabe
JF-Expert Member
- Oct 22, 2017
- 8,781
- 13,444
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanyakyusa ni loudmouths mkuu.Mkuu kimila tuanaoneka tu wengi sababu ya lugha.
Actually wanyakyusa ni kabila dogo sana, tatizo ni lugha.
Mnyakyusa akimkuta mwenziwe, kusalimia kwa lugha nyingine kimila ni kama umemdharau.
Lazima kusalimia kwa lugha ya mama.
Nashukuru ume acknowledge, wanyakyusa ni very hard working.
Ndagha!
Usiwe mvivu wa kutumia ubongo.
Google and check out the facts.
Hata hivyo kutokushirikisha ubongo wako kufikiri(ujinga) ni haki yako ya msingi.
Siyo lugha kinachotuchoresha zaidi ni majina. Unakuta huyu Mwaikambo, huyu mwandambo, huyu mwansansu, huyu Mwanjelwa. Sasa hata kama kwenye Taasisi mpo watatu au wanne mnaonekana wengi balaa.Mkuu kimila tuanaoneka tu wengi sababu ya lugha.
Actually wanyakyusa ni kabila dogo sana, tatizo ni lugha.
Mnyakyusa akimkuta mwenziwe, kusalimia kwa lugha nyingine kimila ni kama umemdharau.
Lazima kusalimia kwa lugha ya mama.
Nashukuru ume acknowledge, wanyakyusa ni very hard working.
Ndagha!
Mkuu huyu mzee kumbe alikuwa na historia kubwa.Mzee Gibbons Mwaikambo almaarufu kama GBM inasemekana alizaliwa tarehe 14 Oktoba, 1938. Mzee huyu wa Kinyakyusa alibobea katika Masuala ya Uchumi akiwa amesoma Shahada ya Umahiri ya Sayansi ya Uchumi kwenye Chuo Kikuu cha Friendship kilichopo Moscow Urusi Mwaka, 1967.
Aidha, alihudhuria Kozi mbalimbali za Utawala wa Bima kikiwemo Cheti cha Utaalamu yaani Certified Insurance Certificate (CIC) na kusomea Masomo hayo Chuo cha BIMA kilichopo Mjini New York Marekani Mwaka, 1970. Aidha, alikuwa Mwanachama aliyebobea kwenye Asasi inayoundwa na Wakurugenzi wa Bima nchini Uingereza (Fellow Institute of Directors-United Kingdom) katika masuala ya utafiti na utawala.
Alibahatika kuoana na Mama Esther Mariki Mwaikambo Mwaka, 1967 ambaye ni Mchaga wa Mwika Kilimanjaro na kubahatika kupata watoto watano akiwemo James aliyerithi jina la Babu yake, Gwamaka na Nkundwe. Mke wake Esther Mwaikambo kwa sasa ni Profesa katika Chuo Kikuu Cha Tumaini Makumira. Ni Daktari Bingwa wa fani ya Udaktari akiwa Daktari Bingwa wa Kwanza Tanzania toka Mwaka, 1969 na amebobea kwenye fani hiyo kwa kumaliza Shahada ya Umahiri ya Udaktari na ya Uzamivu na kufanya Utafiti na Machapisho kadhaa hadi kuwa Profesa. Amepata pia kutunukiwa tuzo ya Dr Martin Luther King na balozi wa Marekani nchini Tarehe 6 Machi, 2013.
Mzee Gibbonce Mwaikambo alianzia kazi kama Meneja wa Bima Iringa mnamo Mwaka, 1970 wakati huo Dkt Amon James Nsekela akiwa Meneja Mkuu wa Shirika la Bima lililokuwa chini ya Wakoloni; Alimrithi Amon James Nsekela Mwaka, 1972 na Kuunda Shirika la Bima la Taifa, wakati Shirika hilo lina Mtaji wa kiasi cha Shillingi milioni 5.5 za Tanzania hadi GBM anaondoka mwaka 1989 inadaiwa aliliacha Shirika likiwa na vitega uchumi vya zaidi ya Sh. 31 bilioni za Tanzania.
Baadaye GBM akahamishiwa Benki ya Rasilimali (TIB) iliyoanzishwa mwaka, 1970 ikimilikiwa na Serikali wakati Asilimia 60% zilikuwa za Serikali moja kwa moja, Asilimia 30% zilikuwa hisa za NBC na asilimia 10% zilikuwa Hisa za NIC; GBM alifanya TIB hadi Mwaka, 1985 akiwa Meneja Mkuu; alifanya kazi na akina Iddi Simba akiwa Mwenyekiti wa Bodi, Amoafo, J. akiwa Mshauri wa Masuala ya Sera, Ndugu A. Kibona akiwa Meneja wa Idara ya Maendeleo na Ndugu Malaki akiwa Mkurugenzi wa Miradi. Mhe Chief Gibbons Mwaikambo, aliteuliwa kuwa Mbunge wa Taifa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwaka, 1980 na kutumika hadi Mwaka, 1985.
Moja ya Mapendekezo yake Bungeni ilikuwa kuishauri Serikali kuunda baadhi ya Kanuni za Kusimamia Ugawanyaji wa fedha za kigeni kwenye Mashirika na Kampuni. Alibainisha kuwa zipo kampuni ambazo utendaji wao mbovu unaathiri Kampuni zingine zinazotegemea Kampuni hizo zisizo na tija katika ufanisi wao. Akatoa Mfano wa Kampuni ya kutengeneza Matairi ya General Tyre ambayo alisema inakaribia kufungwa huku Matairi ya Kampuni zingine hayapewi kipaumbele. Alibainisha kuwa kuna migao mingine ya fedha isiokuwa na Umuhimu.
Ifahamike pia kuwa kwa ubobezi wake wa Masuala ya Bima alikuwa ndiye Mwafrika wa Kwanza kuwa Meneja wa Shirika la Bima kwa Afrika chini ya Wakoloni walioitawala Tanzania na Kuunda Shirika la Bima la Taifa; Kukubalika na Wakoloni haikuwa kazi nyepesi wakati huo. Aidha, Mhe Chief Gibbons Mwaikambo alikuwa ni mmoja ya Wadhamini wa Chama cha Mapinduzi na Mlezi wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi.
GBM alipendwa na Mungu, alifariki mnamo Tarehe 4 Septemba, 1995 baada ya madai kuwa gari yake iligonga mti wengine wakidai ilipinduka na kuzua utata wa Kifo chake.
GBM mbali na usomi wake bado aliheshimika kuwa Chief wa kabila la Wanyakyusa ambapo ililazimika azikwe usiku kama zilivyo desturi za Kabila la Wanyakyusa kuenzi Mazishi ya Machifu yaani “Wanyafyale”.
MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI MHE. CHIEF GIBBONS .J MWAIKAMBO (GBM).
Hiyo ndo historia (kwa ufupi) ya Mzee Gibbons Mwaikambo ambayo nimeikuta sehemu jioni hii, nimetamani nikushirikishe na wewe ili kama ulikuwa na hamu ya kujua mawilimatatu kuhusu Mwaikambo uisome kabla ya kulala usiku huu. Mungu akitupa uzima simulizi kamili kuhusu Mzee GBM zitakujia kupitia kitabu cha "Wanyakyusa Mashuhuri", ambacho nitatamani nikiandike kama itampendeza Mungu.
Huyu ndo Mnyakyusa aliyetuhumiwa kuwa alikuwa na upendeleo sana kwa kuwaajiri kwa upendeleo watu wengi wa Mbeya na hasa Wanyakyusa kwenye Shirika la Bima, na baadaye akatungiwa utani wa kuwa amewahi kusema "Kazi hamna, ila Imbombo jilipo"