Kwa danadana za majaji wetu na maagizo toka juu, hii kesi itakwisha mwaka huu kweli???
Mawakili wa waleta maombi katika kesi ya CHADEMA na wanachama watatu wa chama hicho waliofungua kesi dhidi ya chama hicho wakilalamikia mgawanyo wa mali wamedai upo upotoshaji kuhusu kesi hiyo kwamba zuio ni la siku 14 kitu ambacho wamekipinga.
Akizumgumza na waandishi wa habari mapema leo,Juni, 12,2025 jijini Dar-es-Salaam Gido Thomas Simfukwe kwa niaba ya wenzake amesema kuwa katika kesi ya madai namba 8323 ya mwaka 2025 ya mgogoro wa mgawanyo raslimali dhidi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umma unapotoshwa.
"Amri ya kwanza ambayo Jaji aliitoa ni kuzuia shughuli zote za kisiasa hadi pale kesi ya msingi itakaposikilizwa, amri ya pili amezuia wasitumie mali za chama, kuna upotoshaji unaendelea"
"Kwamba hili zuio limetolewa kwa muda wa siku 14, zuio limetolewa mpaka pale kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi"-Gido Simfukwe, mojawapo ya mawakili wa waleta maombi katika kesi dhidi ya CHADEMA.
View attachment 3366236