GIGY MONEY MMAREKANI BONGO BAHATI MBAYA TUU
Okay kabla hujadiss na kuongea sana tambua kwamba gigy ni msanii
na sanaa ni kucheza na mashabiki wako. Mpoto mashabiki wake ni watu wa heshima na adabu ivo hata akiwa anatumbuiza lazima aonekane mwenye heshima na adabu pia.
Mwanamama Supu (GIGY MONEY) toto mlenda mashabiki zake ni kundi flani la watu flani ambao tukiona msambwanda unarukaruka baasi tunalogeka.
Nyota wa kike Gigy money anaetamba kwa kibao chake kipya cha papa, hua anaonekana akijaribu kufanya wanaofanya wakina nicki minaj na kutimiza ile adha ya kusema BONGO BAHATI MBAYA TUU.
nyota huyu alievuma na ngoma zingine kali kama SUPU anajua dhahiri kutumia limwili flani la mapenzi alilopewa katika kuwanasa mashabiki wake.
Mitindo ya kukatika kwa kujitomasa, kutwerk, kuonyesha kidogo vinono au hata kujishika Papa wakati wa perfomance ni ishara tosha kabisa yulo serious na anachokifanya
Big up sana Gigy