Nasikiaga haachi hela hata laki laki 2 unakula mzigo.
Hivi nyie mbona mnapenda kufuru?
Unaweza ukanunua zinaa kwa laki2? Kichwani panakuwepo sawa kweli?
Kumbuka ni lini uliwapatia wazazi wako ama ndugu zako kiasi hicho cha pesa keshi wakafurahi?
Fikiria mara mbilimbili kabla ya kutia ushabiki kuwa, kusingekuwa na hivyo vyanzo vya uchumi ulivyonavyo, ikatokea ukaenda kwa "tajiri" kuomba kibarua cha laki mbili, ungekifanya kwa miezi mingapi?
Umalaya wa kuuziana mapenzi bei yake ni elfu kumikumi, haizidi hapo.
Hizo laki mbili unazofikiria kununulia penzi la mshindo mmoja, wenziyo wanafikiria watazipata wapi kulipia mahari waoe!
Wacha fikira za kungonoka kwa malaki ya pesa. Utakuja kujutia uzeeni wakati ukiwa tayari kambabu hohehahe usiye na mbele wala nyuma, shabaash.
Thamini kipato chako, jiwekee malengo na akiba kwa ajili ya siku zako za usoni kijana.