Girlfriend wangu anatoa sana namba yake ya simu kwa wanaume wengi

Girlfriend wangu anatoa sana namba yake ya simu kwa wanaume wengi

Joined
Apr 24, 2025
Posts
16
Reaction score
9
Natumai mko wazima wa afya njema, na kwa wale wenye changamoto za kiafya MUNGU awafanyie wepesi mpone haraka na kuendelea na majukumu yenu ya kila siku.🙏

Mimi ni kijana wa kitanzania mwenye umri wa 25 now na ni mwenyeji wa mkoa wa mbeya kyela,ila kwa sasa niko Dar es salaam kimasomo(naomba nisitaje jina la chuo).

Nina girlfriend wangu ambae ana umri wa miaka 20, na yeye yuko chuo hicho hicho ninacho soma but tofauti ni kozi,toka tumeanzisha mahusiano haya now tuna karibia mwaka mmoja,.
Nisiwachoshe ngoja niende kwenye mada moja kwa moja

Kwenye mahusiano yetu tumekuwa na migogoro ya mara kwa mara na sababu kuu ikiwa ni upande wa simu,naweza kusema simu yangu anaikagua na mimi yake naikagua,ishu inakuja vipi kwenye simu yake nakuta anachati na wanaume tofauti tofauti,japo kuwa hizo chat siyo za kimapenzi ila wale wanaume wanaonesha dhahiri nia ya kumtaka kimapenzi,

Sasa ugomvi wetu mimi na yeye ni kuwa KWA NINI ANAWAPA NAMBA ZA SIMU HAO WANAUME WENGINE NA HALI YA KUWA ANAJUA YUPO KWENYE MAHUSIANO ??

Napokea ushauri wowote kwa ndugu zangu wote ambao mmekutana na changamoto kama hizi mlifanyaje au hii ni dalili ya kitu gani…..Naomba kuwasilisha kwenu WAKUU MBALI MBALI 🙏🙏
 
Back
Top Bottom