KERO Giza katika makazi ndani ya manispaa za Shinyanga na Kahama licha ya nyumba hizo kuwa na umeme nyakati za usiku

KERO Giza katika makazi ndani ya manispaa za Shinyanga na Kahama licha ya nyumba hizo kuwa na umeme nyakati za usiku

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Jerry Farms

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
202
Reaction score
167
Hali hii imezoeleka katika manispaa tajwa hapo juu! Na kugeuka maficho ya vibaka na machimbo ya watenda vitendo haramu!

Ni rai yetu kwenu uongozi wa manispaa. Kuja na mpango mkakati wa kutokomeza hali ya ugiza kwa kuzindua angalau kampeni ya nyumba kwa nyumba kuwataka wamiliki kuweka taa za nnje katika makazi yao.

Mamlaka za mipango miji, njooni na muongozo mzuri kuwabana watumiaji wa nyumba katika makazi katikati ya miji. Tungeni hata miongozo itakayo wataka wajenzi wa majengo kuzingatia usalama wa makazi katika maeneo yao.

Msiishie kukaa maofisini, piteni mitaani kagueni utimizwaji wa sheria zenu.

Rai hii haiishii kwa uongozi tu, bali na kwenu wenye nyumba katika maeneo ya mijini wekeni taa za nje kwa usalama wa mali zenu na za raia wapita njia nyakati za usiku. Si ujaja kudai " mnabana matumizi" kwa kutoweka taa za nnje kwa usalama wa milki zenu na makazi salama.

Tunatoa wito chonde chonde, mamlaka za serikali za mitaa pangeni mipango kabambe ya kupambana na giza katika makazi yetu ili kuzuia vitendo ovu nyakati za usiku.

Giza katika makazi mtaa mmoja wapo, Manispaa ya Kahama.

IMG_20241208_204949.jpg

Usalama wa raia na mali zao ni zao la uwajibikaji jumuishi wa jamii, viongozi na mamlaka za usimamizi.
Kwa pamoja tuwajibike,
Wasalaam, Jerry Farms.
 

Attachments

  • IMG_20241208_204949.jpg
    IMG_20241208_204949.jpg
    207.7 KB · Views: 3
Back
Top Bottom