Giza la mchana

Wilfred Ramadhan

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2022
Posts
503
Reaction score
905
Habari wakuu,
Ni mda sasa tangu niwe na mke wangu katika ndoa yetu kuna vitu vingi vimeendelea vingine unameza kama kidume vingine unashare kwa lengo la watu kujifunza au kutoa na kupokea ushauri panapobidi.

Moja kwa moja twende kwenye kiini cha uzi huu,
Mwezi uliopita mke wangu alipokea simu kutoka kwa mama yake (sio mzazi) akapokea maelezo kibao sana niliona akikunja uso wake mzuri kuashiria kama kuna kitu hajakubaliana nacho mara tu baada ya kukata simu ile nikamuulza vipi uko kuna tatizo ?

Akavuta pumzi kwanza na kusema ah sijui niseme vipi ila ni kama tatizo , nikaendelea kumsikiliza pale sasa kilichokuwepo ni kwamba mama yake kamuomba amchukulie mkopo kwenye hizi saccos za kukopesha na yeye hakutaka kufanya vile ila amelelewa na kukuzwa nae na anaona kama akikataa anaweza kuzua maneno mengi yupo njia panda kuamua ilo mimi nilidhani ataenda kama mdhamini ila anaenda kama mkopaji rasmi na mama yake aliwai kukimbia mikopo kadhaa hapo awali ambayo ilipelekea mitafaruko ikiambatana na kushkwa kwa baadhi ya wahusika .

Sasa wife yupo apa anawaza afanyaje mpk anafkria kutoa laki 8 hzo ampe mama yake ambapo ni nje ya natumizi yetu ya mwezi maana tumeshatoa laki mbili na nusu kwa kila familia kila mwisho wa mwezi huwa ni jadi yetu kufanya hivyo

Sasa we kama ndugu yangu nimshauri vipi wife ?
 
Mwambie mke wako amuambie hiyo mama kuwa tayari tuko na deni ambalo alilipata baada ya mdhamini kumkimbia na bado anahangaikia kulilipa

Mwambie kuna mtu alimdhamini lakini mwisho wa siku akasepa kamuachia shuka, waliomkopesha wameanza kudeal na mdhamini na sasa anaenda mwezi wa pili huu analipa kidogo kidogo
 
Niliwaza hivi pia ila mama kakaza ndo kwanza katuma mtu leo achukue passport za wife
 
Huwa kwenye kukopa inakua hivi yule mama anadaiwa FINCA na huko tayari hawezi kwenda kuchukua ndio maana katafuta kampuni lingine wife akamchukulie na mama ni mzoefu wa mikopo anazijua trick trick na vigezo kuhusu hizi kazi
Amgomee kwa maslahi yenu...maneno kitu gani Kwani!!..nawewe unashindwa kuongea na mkeo vizuri??.?embu ongea nae bana kabla hamjakutwa na kitu kizito..shauri zenu
 
Amgomee kwa maslahi yenu...maneno kitu gani Kwani!!..nawewe unashindwa kuongea na mkeo vizuri??.?embu ongea nae bana kabla hamjakutwa na kitu kizito..shauri zenu
Apa inabidi iishe kinamna hii maana wife analia tuu apa
 
Una umri gani?
 
Amwambie tayari naye anamkopo na niwa miaka 5 na hana sifa yakukopa tena.
Anadai kwa kusema uku unakoenda kunikopea hawajui kitu kukuhusu ko usiogope alimwambia hivo maana mwanzo niliwaza ii kitu nikamshauri wife
 
Kwanza huyo mama anawaona mna pesa maana kutoa laki 2.5 sio mchezo tena kila mwezi.wanawashauri asichukue mwambe hawezi kufanya kwani hali yenu sio nzuri.
 
Apa inabidi iishe kinamna hii maana wife analia tuu apa
Analia nini sasa au ndiyo anamiaka 20? Embu kueni na mkeo, huyo Mama mjini itakuwa ee anawapa pressure, kwani maneno yakitokea nyie mtashindwa akuishi bila wao? Kataa na kwao msiende.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…