AREA 255
Member
- Sep 17, 2014
- 5
- 0
Hapana shaka mfuko wa taifa wa Bima ya afya ni hitaji la msingi la ulinzi wa afya kwa wananchi wote, katika kujenga taifa lenye siha linaloweza kupambambana na adui maradhi ili kujenga jamii iliotayari katika kujenga uchumi endelevu kuelekea uchumi wa kati kamilifu kama maelekezo ya dira ya maendeleo ya 2025 yanavyo tanabaisha.
Afya ndio msingi mkuu wenye kujenga jamii inayojitegemea, jamii yenye ustawi unaoendana na ukuaji wa teknolojia katika dunia yenye ushindani, katika karne hizi ambazo zinatajwa kama dhama za maendeleo ya juu ya utandawazi katika kuifanya dunia kuwa sehemu moja (yaani dunia kama kijiji)
Takribani wiki kadhaa sasa, mfuko wa Taifa wa bima afya na wadau wake wameanza kutekeleza agizo la waziri wa afya Mh. Ummy Mwalimu la kusitisha matumizi ya fomu namba 2C. Kutoka na changamoto kadhaa zilizotajwa kama sababu za kusitisha utoaji huduma kwa kutumia fomu namba 2C ni udanganyifu unaofanywa na wamiliki wa maduka washirika ya dawa kwa kushirikiana na wataalamu wa hospitali za umma na binafsi, kama vitendo viovu vya kuhujumu Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya, wataalamu wa afya binafsi na wa umma wamekuwa wakitoa kipaumbele kwenye matumizi ya fomu namba 2C kinyume na malengo ya NHIF, wakishindikiza wagonjwa wakachukue dawa kwenye maduka binafsi yaliopo nje ya hospitali na vituo vya afya yenye mahusiano na wao.
Ikumbukwe kwamba Fomu namba 2C ni fomu maalumu ya NHIF ya kuchukulia dawa kwenye maduka washirika nje ya kituo cha kutolea huduma za afya.
Katazo hilo limewekwa bayana na Mh.Waziri wa afya Mh. Ummy Mwalimu huku akijinasibu kuokoa mabilioni ya shilingi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya kutoka hospitali ya taifa ya Muhimbili siku chache tu mara baada ya kuanza kutumika kwa utekelezaji wa katazo hilo.Wakati tukiendelea kulitafakari hili la kusitisha matumizi ya fomu namba 2C, August 1, 2022. Utaratibu mpya wa matibabu unaanza kutumika ukizuia idadi ya mahudhurio kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwa mgonjwa yasizidi mara tatu kwa mwezi isipokuwa kwa mahudhurio ya dharula.
Utaratibu huo pia ulisitisha huduma za moja kwa moja isipokuwa kwa vibali maalum kwa wagonjwa wote wanaohitaji kufanyiwa vipimo vya MRI, CT SCAN, Colonoscopy, HBA 1C, OGD, USS na ECHO. Udanganyifu ukitajwa kwa mara nyingine kama hoja ya msingi ya utaratibu huu ulioanza kutumiaka August 1, 2022.
Lakini siku tatu baadaye Augost 3, 2022, Waziri wa afya Mh. Ummy Mwalimu anatangaza kusitisha utaratibu huu, huku akisisitiza wadau wakutane kuangalia changamoto hii ili kupunguza usumbufu kwa wanachama wa mfuko wa Taifa wa Bima ya afya wanaopokea huduma kutoka vituo mbalimbali vya afya vya umma na binafsi inchi nzima.
Usitishaji wa matumizi ya fomu namba 2C pengine kwa upande mmoja haukuzingatia uhalisia wa uwezo wa hospitali zetu na vituo vya afya katika kutimiza wajibu wa utoaji dawa kwa wagonjwa. Zaidi usitishaji huu ulilenga katika kulinda mfuko wa Bima afya, ambapo takwimu zinatanabaisha kuwa umekuwa ukipungua thamani kila baada ya mwaka.
Inajulikana wazi hali ya upatikania wa dawa si ya kuridhisha hata kidogo husausani maeneo ya pembezoni hasa nje miji na majiji makubwa katika hospitali zetu za umma, ukiritimba na miongozo mirefu ikianzia kwa MSD (ususani kitengo cha manunuzi) michakato ya usafirishaji isiozingatia uharaka na uhitaji mkubwa wa dawa mahospitalini, uaminifu mdogo wa watumishi katika kufanya kazi wa weledi na kulinda rasilimali fedha ya Taifa.
Katazo hilo la fomu namba 2C limepelekea kuibua sitofahamu kwa wananchi husasani wanachama wa NHIF, ambao takwimu zinaonyesha ni asilimia nane (8%) tu ya watanzania wote, kwani katazo hilo halikuambatana na mbadala kama endapo itatokea mgonjwa kushinda kupata dawa iliopendekezwa na daktari ndani ya kituo cha afya au hospitali, je mgonjwa afanye nini? Zaidi, Waziri Ummy alisisitiza ni jukumu la hospitali au kituo cha afya kumtafutia mgonjwa dawa.
Kisa hiki cha fomu namba 2C kinashabiana na hadithi ya Bunge la Tanzania miaka kadhaa nyuma lililopandisha bei ya mafuta ya taa kwenye bajeti ya serikali eti kuzuia kile kilichoitwa uchakachuaji wa “petrol na deseal” pasipo kuzingatia mtumiaji wa mafuta ya taa ni wananchi wa hali ya chini kabisa.Hii ni taswira hofu kwa mfuko wa bima afya, katika harakati zake za utendendaji wake ikiwemo miongozo kadhaa isiomaliza changamoto za uhitaji kwa wateja wake kama utambuzi wa wategemezi usiondana na mazingira halisi ya kiafrika na tamaduni zake.
Maswali kadhaa yanaweza kuibuka ndani ya katazo hili la fomu namba 2C, endapo fikra zako zitasafiri maili kadhaa mbele kwamba serikali inajaribu kujitisha na kinyago chake kwa kushindwa kuthibiti watumishi wasiokuwa waaminifu ndani ya mfuko wa Bima afya na kupelekea kusitisha matumizi ya fomu namba 2C tena kwa notisi ya muda mfupi sana. Je serikali imeshindwa kuthibiti vituo vya afya na hospitali zinazofanya udanganyifu ambao kila kukicha zinaendelea kusambaa kama uyoga kila kona ya nchi? Ambazo miongoni mwao kwa kiasi kikubwa zinahusishwa katika kufanya udanganyifu kwa kuongeza idadi ya dawa katika fomu ya mgonjwa baada ya matibabu.
Wakati mwingine wataalamu wa afya kwenye baadhi ya vituo vyao, wamekuwa na tabia ya kuwapumzisha wagonjwa kwenye vituo hivyo hata kwa ugonjwa usiohitaji mgonjwa kupumzishwa kwa lengo tu la kuongeza gharama kwenye bili hasa kwa watejea wanaotumia bima za afya ikiwemo NHIF. Hiki ni kichefu chefu kisichovumilka na ni budi serikali ichukue hatua stahiki ili kujenga taswira chanya kwa wanachama wa NHIF na kunusuru kufilisika kwa mfuko huu ambao ni tegemeo kwa watanzania wengi.
Katazo hili la matumizi ya fomu namba 2C, huwenda lisiwe muarobaini wa kudumu wa kumaliza tatizo endapo hatua stahiki na utekelezaji wa teknolojia hautapewa kipaumbele. Mabadiliko ya kisera na kimuundo hayana budi kupewa nafasi sambamba na ushirikishwaji wa wadau katika mabadiliko ya kanuni na mikakati mbalimbali ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya.
Vile vile taasisi hii ni vyema ikaondoa dhana kutengeneza faida katika utoaji wa huduma kama ilivyo makampuni mengine ya bima bali lijikite katika kuleta ufanisi wenye weledi na kuzifanya huduma kuwa takwa la msingi kwa wananchi wote katika kupata huduma bora na za uhakika za afya nchini.

Upvote
2