SoC04 Giza lenye Mwanga

SoC04 Giza lenye Mwanga

Tanzania Tuitakayo competition threads

mcmane

New Member
Joined
Jun 26, 2024
Posts
1
Reaction score
1
Nashiba nikionja ni Kila natapika!!

Namshukuru aliye asili yangu Kwa pumzi na uweza wangu wa kupata na Kutoa taarifa Kwa jamii ya watanzania.

Nyumba yangu imejengwa msingi tu,Haina Kuta,haija pauliwa ,natafuta mafundi,nawapata wananiambia wao hufanya kazi kwenye Giza.Je! mnaonaje!! Wananiambia niwape kazi ila kabla wanataka niwape yafuatayo;

1.Tupe muongozo imara ,unao onesha namna Bora ya sisi kuishi na kufanya kazi Kwa uhakika na weledi,Kisha baada ya miaka mitano njoo uone nyumba Yako itakavyo kuwa Bora,,Kivipi? Nauliza,,muongozo ni katiba ambayo itaweka wazi namna Bora ya kuenenda vile utakavyo na sisi tutakvyo bila kulaumiana.

2.Hakikisha tuna vifaa vya kiteknolojia pamoja na internet ya kutosha.Jamani mafundi!! Nitavitoa wapi? Usiwaze Nenda Kwa majirani au Kwa mtu yeyote unae muamini mfano kule Kwa jamaa Yako MKorea kusini , kisha wapeleke watoto wako Kwa muda hata wa miaka 20, wajifunze shule za kiteknolojia ikiwemo uundaji pamoja na matumizi ya vifaa vya kiteknolojia.Ili sisi tukianza ujenzi wa nyumba Yako tusihangaike,vifaa na maarifa.

3.Tuambie miiko na tamaduni za msingi wa jengo lako,,na kama umeziharibu usiogope kuanza upya.Laaa hasha! Nyie mafundi yaani nibomoe msingi wa jengo Kisha nianze upya kisa tamaduni? Ndio! tamaduni zako ni kiungi na msingi wa maadili ya ujenzi wa nyumba uitakayo. Kwakuwa uzazi wako hauna ukomo,basi hakikisha kizazi kijacho kikute misingi Bora ya kimaadili.China ni Moja ya nchi zinazo Linda Mila na tamaduni zao,lakini hata Moja ya watoto wako yule mchaga anajitahidi sana,Sasa fanya watoto wako wote warudi kwenye tamaduni zitakazo wafanya wawe imara.

4. Je ,siasa Yako ikoje? Mimi siyo mwanasiasa!! Hapo ndipo unapo kosea ,siasa ni jumla ya maisha tunayo ishi na shughuli tutendazo Kila siku. Siasa Ina beba vitu vingi shughuli za uchumi, elimu nk, siasa siyo uwongo Wala utani Bali ni mfumo ambao watu wanautumia kutengeneza namna ya kuendesha maisha.

ANGALIA MOVIE MOVIE INAITWA "LIKE STAR ON EARTH"
Sometimes we can see what is not there and sometimes we can not see what is there.Hujashindwa maana unaweza onekan umeshindwa kumbe njia uliyo pita ndio siyo sahihi.

UFUPISHO
Ili tujenge Tanzania Bora na imara
1. Kama watanzania, tusibishane kuhusu katiba,tuangalie kama Kuna marekebisho tuyafanye.
2. Elimu ya sayansi na teknolojia iwepo tena Kwa ufanisi sio maneno tu.
3. Turudi kwenye tamaduni zetu, ili tuweke kujenga vizazi vyenye kufuata miongozo ya nchi yetu.
4. Siasa yetu iwe safi, na ikiwezekana siasa usifanywe kama biashara, ya watu kutajirikia, hapa tutapata viongozi siyo wafanya biashara.

MWISHO
Shule ziwe siliasi kufundisha tamaduni za nchi.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom