Pre GE2025 Giza limetanda kwa wapinzani wa nchi hii, ni ngumu kushika dola

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nje ya mada kiongozi,Eti DC wa Longido kakosea wapi kwenye hotuba yake mpaka uteuzi wake umetenguliwa?

Kama mambo ndio haya sioni haja yakusema vyama vya upinzani huku ukweli ni kuwa kuna watu wanapanga matokeo
Mamlaka ya uteuzi ndiyo unajua zaidi.
 
Na wakati wa Maguuli ulikuwa unaandika uharo kama huu ? au kwa sasa shungi linakuchanganya?
Wakati ule tungeandika pia ungesema tunafurahia wapinzani kuumizwa au siyo?Shungi ni vazi tuh,hata wewe unaweza kuvaa likakupendeza na sisi tukakusifia vile vile.
 
Mamlaka ya uteuzi ndiyo unajua zaidi.
Sawa kiongozi lakini nasikia diwani hana uwezo wowote kwenye uchaguzi kushinda bila mkono wa serikali (ni sehemu kidogo ya kilichosemwa japo sijanukuu kama ilivyo ni tafsiri yangu lakini ujumbe ni sawa)

Sasa kama hiko hivyo wapinzani unategemea ata wangekuwa imara kama unavyotaka bila utashi wa hawa wenye kupanga matokeo unahisi kuna mabadiliko au tusubiri nguvu ya watu(never) au majeshi yafanye yake sio?
 
Kama aliyazungumza hayo na mamlaka ya uteuzi imemtengua basi ni wazi kuwa hayo aliyoyasema ni yake,ameyazua ndiyo maana akatumbuliwa,angeachwa maana yake hicho alichokisema kingekuwa ni kweli.
 
upinzani wa bongo ni usanii mtupu wapishe watu wenye akili zao waongoze nchi ccm daima mbele nyuma mwiko
 
Hakika umeongea kitu chenye maana kubwa Sana.
Ndio hali halisi mkuu, vyama vingi vinavyoanzishwa huwa vinakua na nguvu sana pale mwanzoni ila kadri siku zinavyokwenda na miaka kupita nguvu inapungua kwa maana hawapendi kufanya recruitment ya damu changa ili ziendelee kuvipa nguvu vyama vyao.

Na badala yake daily tunawaona wale wale ambao tumewazoea (hadi wanapoteza mvuto) na kiuhalisia hii ni moja ya indicator muhimu sana kwamba unapotaka mabadiliko lazima utuoneshe kwa vitendo kuanzia kwenye taasisi yako.

Sio unahubiri tu mabadiliko wakati wewe mwenyewe huwezi kuyaishi hata angalau kidogo tu... vyuoni kuna vijana kibao ambao wakifanyiwa recruitment wanakua na uwezo wakuja kuwa watu bora sana na kutupeleka kwenye mabadiliko ambayo tunayahubiri kila siku.

Na vijana msikubali kuweka nchi rehani kwa mihemko na mahaba au sifa za kijinga ila ni muhimu kila mtu aweke hayo yote pembeni na afikirie kwa wakati wake kabla ya kufanya maamuzi.

Najua asili ya mwanadamu ni kutamani vitu ambavyo hajawahi kuwa navyo ila once akivipata ndio anagundua kumbe hakuna maajabu yoyote na ndivyo ilivyo kwenye hili.

Ila kila mara tunaposumbuliwa na hiyo asili lazima tukumbuke usemi huu wa waswali unaosema kwamba ZIMWI LIKUJUALO HALIKULI LIKAKWISHA.
 
Je vipi waliojaliwa roho ngumu mbaya isiyo jali na yenye ujasiri?
 
Kama aliyazungumza hayo na mamlaka ya uteuzi imemtengua basi ni wazi kuwa hayo aliyoyasema ni yake,ameyazua ndiyo maana akatumbuliwa,angeachwa maana yake hicho alichokisema kingekuwa ni kweli.
Lakini yeye ni credible source licha ya mamlaka kumtumbua haifanyi kilichosemwa kuwa cha uongo.

Kumbuka hiyo mamlaka ndio mara ya kwanza ilimpa baraka ya kusimama kama mwakilishi wa mamlaka za juu Longido kwahiyo kuna direct link kati yake na mamlaka za juu hakuna namna anaweza sema uongo
 
jamaa anajua kila kitu anajitoa tu ufahamu
 
Je vipi waliojaliwa roho ngumu mbaya isiyo jali na yenye ujasiri?
ni pepo tu hilo, ñjoo ufanyiwe maombi tu na utakua jasiri kama Simba, lakini huru, usie na hofu, mwenye nguvu, maarifa na maono ya mbali kabla ya hatar 🐒
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…