GK: Nikipewa nitumie "beef" ya Diamond na Ali Kiba kutengeneza pesa watakua mabilionea.

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
Rapper mkongwe nchini, King Crazy GK amesema akipewa fursa ya kutumia bifu ya Diamond na Alikiba, atawafanya wawe mabilionea.

Rapper huyo amedai kuwa atahakikisha wawili hao wanaongeza uhasama zaidi kuliko hata ilivyo sasa. Wakati mengi yakiendelea kuzungumzwa kila kukicha kuhusiana na wawili hao , GK amesema angewahakikisha wawili hao wanapiga mkwanja wa kutosha.

“Ni upinzani mzuri kama nikipewa mimi kutengeza pesa watakuwa mabilionea wale mabwana,” anasema. “Kwanza nitaongeza conflict, ule mgongano sitoupunguza, nitauongeza, nitazidi kuuvibrate uwe mkubwa watu wa waufeel. Sasa upo upinzani kwa Kiba na Diamond zaidi personal, sasa mimi nitauweka watu wauvae yaani wakikutana pale inakuwa noma,” ameongeza.

Crazy GK anadai angepambana kuwe na mipango ya kuhakikisha wawili hao wanapiga hela nyingi ikiwemo kufanya show uwanja wa taifa.

MY TAKE: Gk kapatwa na nini?!,
 
GK naye,kaishiwa kweli!!

Mondi hana bifu na Ali Kiba, bali Ali Kiba anataka kutumia ma haters wa domo ambao ndo mashabiki wake ili kuendelea kuwepo juu ki muziki. Ali Kiba pia ana pambwa na media hasa ya mawingu ambao wanataka tuu domo ashuke, (japo imesha shindikana).Japo Kiba si msanii mbovu ila Wana m overhype Kiba sana hawa jamaa.
*huu ndo ukweli na ukweli uta tuweka huru
 
Mwisho wake huwa nikupigana mana watahamia kwenye matendo ya kweli 2pac na big.
 
Hakika huu ukweli upo wazi lakini watu wanaupinga, Thanks Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…