A
Anonymous
Guest
Msimu huu wa mvua sisi wakazi wa Goba tumekutana na changamoto kubwa ya ubovu wa miundombinu.
Mtaa wa Bonde kati ya Shule ya Living Minds/Kanisa la RGC na Matosa umeharibika kabisa, magari ya shule asubuhi yanapata changamoto kupita, watembea miguu wanazama matopeni na bajaji hazipiti kabisa.
Goba makazi yanaongezeka kwa kasi lakini miundombinu inabaki nyuma sana, Wilaya na TARURA mvua zikiisha wachukue hatua ya kuboresha mitaa yetu, hasa kuweka mitaro vizuri. Huko bondeni walileta greda mwezi machi ila marekebisho yote haya bure kisa kutozingatia mitaro. Mvua moja, mtaa ukawa mfereji. Tena majaribio yaliyofuata ya kujaza mashimo na takataka si utatuzi wa shida bali ni uchafuzi wa mazingira.
Serikali iache kutiba dalili tu na kupoteza hela kwa suluhisho za muda mfupi.