KERO Goba Center karibu na Shule ya Living Minds ikinyesha mvua Mtaa unageuka kuwa Mto

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Msimu huu wa mvua sisi wakazi wa Goba tumekutana na changamoto kubwa ya ubovu wa miundombinu.

Mtaa wa Bonde kati ya Shule ya Living Minds/Kanisa la RGC na Matosa umeharibika kabisa, magari ya shule asubuhi yanapata changamoto kupita, watembea miguu wanazama matopeni na bajaji hazipiti kabisa.

Goba makazi yanaongezeka kwa kasi lakini miundombinu inabaki nyuma sana, Wilaya na TARURA mvua zikiisha wachukue hatua ya kuboresha mitaa yetu, hasa kuweka mitaro vizuri. Huko bondeni walileta greda mwezi machi ila marekebisho yote haya bure kisa kutozingatia mitaro. Mvua moja, mtaa ukawa mfereji. Tena majaribio yaliyofuata ya kujaza mashimo na takataka si utatuzi wa shida bali ni uchafuzi wa mazingira.

Serikali iache kutiba dalili tu na kupoteza hela kwa suluhisho za muda mfupi.

Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
​
 
Tukiwa nje ya nchi mtutaki mnasema tumetumwa na mabeberu haya .Mliopo na mafisi CCM waambieni wajuwe kutatua maendeleo kwa wizi wa uchaguzi ndio maji yatajiongeza
 
Hali ni kama kwetu hapa Mbeya ila sasa sisi Mbeya vumbi ndilo linatutesa. Sasa hivi tumeacha kuita Green city ila tunaita VUMBI City
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…