Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu
Huko Goba, wagombea wa CHADEMA wenye kazi rasmi wameenguliwa kwa madai kwamba shughuli zao hazitambuliwi kama kazi rasmi za kiuchumi.
Hii ni tofauti na wagombea wa CCM ambao, licha ya kujitangaza kuwa hawana ajira (jobless), wamepitishwa kugombea. Hivi karibuni, mgombea wa CHADEMA katika mtaa wa Kisauke ambaye ni dereva, aliwekewa vikwazo na kuenguliwa kwa sababu udereva haukutambulika kama kazi rasmi.
Soma Pia: Mgombea wa CCM aliyeandika amezaliwa mwaka 2024 kwenye fomu, aripotiwa kupitishwa kugombea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Hali kadhalika, mgombea mwingine wa ujumbe wa serikali ya mtaa eneo hilo hilo, ambaye ni mfanyabiashara wa Kariakoo, aliwekewa kizingiti kwa sababu ujasiriamali pia haujatambuliwa kama kazi.
Cha kushangaza, mgombea wa CCM ambaye alitangaza hadharani kuwa hana ajira yoyote, alipitishwa kugombea, kinyume na Kanuni za uchaguzi za Serikali za Mitaa, hasa Kanuni ya 15(d) na 17(5), zinazotaka mgombea awe na shughuli rasmi ya kumwingizia kipato.
Inaonekana msimamizi wa uchaguzi wa Goba anaona udereva sio kazi, ujasiriamali sio kazi, lakini kukosa ajira ni kazi!
Na bado Waziri Mchengerwa, licha ya kufahamu changamoto hizi, ameshauri wagombea walioenguliwa wakate rufaa iwapo wanaona wameonewa.