Goba vs Kigamboni: Wapi ni pazuri zaidi?

Nenda tu goba asee huku kigamboni usije kabisaaa tuachie tukae na mamwinyi wetu. Alaf kigamboni pa kishamba sana bado kunasehemu Zinajaa maji alafu sio sehemu salama kuishi ww nenda goba
 
Kigamboni bor zaidi ...changamoto pekee inayofanya watu wapashushe thamani ni namna ya kufika kigamboni ni either kivuko,darajani au uzunguke njia ya kijichi au kongowe

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio wapashushe thamani wao ndio hawana thamani yaani mwanaume unashindwa kulipa hela ya daraja au hela ya kivuko dah inasikitisha sana. Watu wengi wanaogopa gharama ila ukipiga hesabu vizuri bado kigamboni ni sehemu nzuri kwa watu jasiri.
 
Kigamboni kumekaa kushoto sana
Kwa mishe mishe za mjini goba Ni hub nzur Sana ya kua connected na harakati
Hamna sehemu iliopo mbali (inategemea wewe unatokea wapi) Sasa wewe wa goba unakuja posta namimi wa mjimwema naenda post nani yupo mbali? Mimi navuka maji tu nipo posta wewe mpaka ufike posta ni au kariakoo ni mbali sana
 
[emoji23][emoji23][emoji23] hicho kiwanja Cha ukubwa huo unapata Kwa M1 ni kigamboni ipi hiyo kinapatikana maana Mimi sijawahi kusikia
 
Kigamboni watu wanai under estimate lakini ni sehemu nzuri sana ya kufanya settlement
• Kibiashara Unaweza ukanunua maeneo yaliyo karibu na Barabara au baharini then ukafikiria kitu Cha kuwekeza
•kimakazi napo panafaa sana kutokana na Hali ya hewa

Siku Barabara ya lami ikipita kote kuanzia mwasonga - buyuni na Kimbiji mpaka ije iungane na Cheka. ..ndipo watu wataijua thamani iliyopo kigamboni
Ni sehemu potential sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…