Mi nachoamin mungu yupo
Ila wazungu waliwashika babu zetu pabaya
Umetuimia njia gani au kipi kimekufanya wewe uamin Mola muumba yupo ?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mi nachoamin mungu yupo
Ila wazungu waliwashika babu zetu pabaya
nilitegemea niliyemnukuu anijibu swali hili lakini kakimbia
hapa ndipo watu kama sisi tunapokuwa na mashaka na neno mungu
tunaamini kuna one highest power ambayo tunaiita the creator,huyu muumba hana intermediaries wa kutuma salamu zake kwa watu
mungu ni concept iliyotengenezwa na watu,ukiangalia almost kila ethnic group wana mungu wao ambaye anatofautiana na group jingine....
Hakuna Mungu mmojaHalafu tukiwaambia mna matatizo ya akili,mnalalama.
Hivi ushawahi kujiuliza kwanini watu wanamuelezea Mola kivyao hali ya kuwa wanasema wana muamini Mungu mmoja ?
hakuna mungu mmoja
wa kikristo ni tofauti na wa kihindi
wa kiislamu ni tofauti na wakichina
Mola anaweza kuwa mmoja lakini miungu ipo mingi,mfano allah na yehova wako tofauti kabisa kuanzia paradiso hadi jehanamu zaoHapa kuna hakika ya mambo yalivyo na kuna maoni ya watu. Ama kuhusu hakika ya mambo kwayo ndio ukweli ulivyo Mola muumba ni mmoja tu.
Ni yule aliyekupa.akili, macho, miguu, midomo, pumzi n.kmungu gani ambaye unadai yupo?
allah?yehova?yesu?zeus?Ra?Horus?
Nitajie jina lake kati ya hayo niliyokutajiaNi yule aliyekupa.akili, macho, miguu, midomo, pumzi n.k
Ok let's say there's creator of universe,why you conclude he/she is God and not otherwise?Habarini wa GT.
Kumekuwa na mgongano wa mawazo kuhusu uwepo na ithibati ya Mungu.Naomba niseme ya kuwa mgongano huu haujaanza leo wala jana bali ni karne kwa karne zimeshapita. Nitaanza kwa kusimulia visa kadhaa kabla ya kujenga hoja.
Mwanafalsafa Plutarch(myunani) aliyekufa mwaka 120b.c na mwandishi wa habari za wayunani na warumi katika kitabu chake kinachoitwa "Parallel lives of illustrious Greek and Romans"aliandika ya kuwa Kuna miji isiyo na kuta, wala vitabu isiyo na mfalme, wala nyumba wala hazina wala mahala pa kuchezea michezo; Lakini hakuna mji usiokuwa na hekalu la Mungu(mungu fulani) hakuna mji huo na hutapata kuuona.
Mwana sayansi wa elimu ya viumbe Athanasius Kirchner(1601-1680) alikuwa na rafiki yake ambaye alikuwa anapinga uwepo wa Mungu. Kuna siku huyu rafiki alimtembelea Kirchner, Alikuta Kirchner ameshika tufe lenye sura ya dunia, kutokana na ustadi uliotumika kulifanya tufe hilo Jamaa akamuliza Kirchner"Nani aliyeufanya mfano wa dunia hivi? Kirchner akajibu Hakuna mtu, umejifanya wenyewe.Jamaa akasema acha kunichekesha aliyeufanya mfano huu lazima awe mstadi mkubwa, Jinsi gani Kirchner akahoji? Hutaki kukubali ya kuwa mfano huu dhaifu wa tufe la dunia umejifanya wenyewe lakini unakazana kuwa dunia hii kubwa (universe) umejifanya wenyewe.
Kuna watu wa aina bado wapo.
WHAT'S INVISIBLE THAT CREATES WHAT'S VISIBLE.
Kama kitu hakithibitishiki kwa milango ya fahamu (pua,ulimi, macho, ngozi,masikio) haifanyi kitu hicho kisiwepo.Kuna ya vitu hauwezi kuthibitisha kupitia milango ya fahamu lakini vipo katika mazingira yetu.Ili kuthibitisha uwepo wa mambo/vitu hivyo tuna angalia athari yake (Low of course and effect)Hapa nitaweka baadhi vitu/mambo hayo ili kuelewa vizuri low hii.
These facts are not all of one kind, some are material and some are non material. We shall mention here a few of them.
Electricity, Gravitation, Magnetism, Invisible radiation, Intelligence, Love, Hate, Determination. and so on.......
Hivi ni baadhi ya vitu/mambo hatuwezi kuthibitisha kwa milango yetu ya fahamu lakini vipo, Tunamini vipo kwasababu ya athari zake.
Kwa hiyo; hoja ya kuwa Mungu hayupo kwa kuwa hatuwezi kumthibitisha kwa milango yetu ya fahamu inakufa/haina uhai kwa scenario hii.
Mungu hujibainisha kwa viumbe wake kupitia alama/sign mbalimbali rejea paragraph za juu hapo(matukio hayo mawili).
Karibuni
Wewe unaemuamini anaitwaje?hakuna mungu mmoja
wa kikristo ni tofauti na wa kihindi
wa kiislamu ni tofauti na wakichina
Unajua wewe unachekesha sana nan alikuaminisha kuwa kuna creator ambaye ni spirit? ebu tuanzie hapo naona umahanyika tuwapi nimekwambia uamini!!!!!!!!!!
hebu nikupe shule kidogo
mimi naamini uwepo wa supernatural power/divine intelligent (which i believe created everything and i do believe this creator is just a spirit)
siwezi kuprove existence ya hiyo spirit,it is just my own thinking
wao,probably na wewe wanaoamini uwepo wa mungu anayezungumza na watu wanahitaji kutupa ushahidi wa huyo mungu kuwa ameongea nao na kuwatuma kuwaeleza binadamu ujumbe flani
i do not have any burden of proof,mungu wanaomuelezea kwenye vitabu vyao/vyenu ni kiumbe chenye tanuri la moto,ana palace lenye kila raha....
soma vizuri uelewe nilichoandika hapa ili uje na hoja mpya ambayo nitajibu
Wewe ndio sio muelewa,unachokiamini wewe ni tofauti na wanachoamini wenzako,wenzako wanaamini Mungu ila wewe hauamini Mungu unaamini tofauti na unasema Mungu ametungwa tu na watu,sasa wewe kama hauamini Mungu kuna haja gani ya kutaka kuthibitishiwa kitu kuhusiana na Mungu hali ya kuwa hauamini huyo Mungu?mzee we mgumu sana kuelewa
kuamini uwepo wa muumba ni kitu kimoja lakini kusema amekutuma kuandika kitu flani ni jambo jingine
kuamini ni kitu kimoja lakini kusema amekuambia kitu flani jambo jingine
nachokataa mimi ni kwamba eti kuna mtu anasema kaongea na huyo mungu
unaposema umeongea naye inabidi uprove pasipo shaka kuwa umeongea na ye
kuamini yupo au hayupo haina tatizo
tatizo ni kutuaminisha kuna watu wameongea naye,lakini hakuna ushahidi wowote
nachoamini mimi ni simple,sijawahi kusema nimeongea na creator,siku nikisema hivyo itabidi nitoe ushahidi wa kuongea naye
vitabu vya dini vimemdescribe mungu wao kama mtu mwenye kumiliki tanuru la moto
mfano mohamed anasema alikuwa anaongea na mungu wake anayeitwa allah mapangoni akiwa peke yake,how the fvck you believe that garbage!!!!
kama hujaelewa hapa sijui naweza kukuelewesha vipi
Labda tuna mitizamo tofauti juu ya hii dhana ya muda.Hapa nasema chochote kuhusu hili.
Mola muumba alikuwepo kabla ya chochote kuwepo kabla yake na atakuwep kabla ya chochote kuwepo baada yake.
Suala la muda nilishawahi kujadiliana na mtu mmoja katika jukwaa hili lakini upingaji wake ulikuwa wakitoto na kucekesha sana.
Mola wetu aliumba muda,na Mola wetu ameapa sana kwa muda. Na akatuwekea hali na viumbe wengine ili kuutambua muda,kudhibiti miaka na kudhibiti mahesabu.
Kwa ufupi Mola hajatanguliwa na wakati .....
Nipo ....
Hapo ndipo palipo na tatizo,unaposema mtu akiamini Allah huna tatizo naye wakati huyo Allah kabla ya kuaminiwa kwanza ameelezewa na watu ambao wamepata maelezo hayo kutoka kwa Allah mwenyewe na si kwamba wamejitungia tu wenyewe ila wewe ajabu unasema huna tatizo mtu akiamini Allah!hebu niandike katika lugha ambayo mtu kama wewe utanielewa unless umeamua kuleta ubishi wa kijinga;
ukiniambia unaamini yupo allah ambaye ni mungu wako sitakuwa na tatizo,it is just imani
lakini ukiniambia umeongea na allah hiyo sio imani tena,ni kitendo...sasa unachotakiwa ni kuprove kwangu kuwa umeongea naye na amekutuma uniambie unayoniambia..is that too old for your brain to grasp?!!!!
Ahahahaha aaah, aiseee we jamaaa ilaa safi otherwise Naomba Mungu Akuoongooze huo msimamo wako hata ikujiee miujiza ya Aina ganii utasimama palepale.Ahsante kwa kunitajia Plutarch. Hivyo vitabu viwili vyote ninavyo na nimevisoma. Umenirudisha kuangalia kabati langu la vitabu vya historia ya enzi hizo.
Plutarch alikuwa mwanahistoria mzuri sana, hata Shakespeare alipoandika tamthiliya na michezo yake kuhusu Warumi, alimtumia Plutarch sana.
Tunaweza kusema Plutarch ni Shakespeare wa Shakespeare, kwa wasiomjua, lakini wanajua umuhimu wa Shakespeare, hilo linaweza kumuelezea umuhimu wake.
Lakini hilo halimfanyi Plutarch awe hawezi kukosea. Kuna mengi sana hakuyajua ambyao sisi tunayajua.
Habari ya kitu kujifanya chenyewe au kutojifanya chenyewe haithibitishi uwepo wa Mungu.
Kwa sababu, hata kama ulimwengu haiwezekani kuwa umejifanya wenyewe, hilo halimaanishi automatically kwamba umefanywa na Mungu.
Inawezekana ulimwengu haujajiumba wenyewe, na wala haujaumbwa na Mungu.
Na narudia tena, habari ya "kitu complex lazima kina aliyekifanya" inatuonesha Mungu hawezi kuwepo, kwa sababu Mungu naye ni complex na atahitaji muumbaji wake, na muumbaji wake atahitaji muumbaji wake, ad nauseum, ad infinitum.
View attachment 906505
Sijapinga uwepo wa Mungu kwa sababu haonekani, hagusiki, hanusiki etc.
Napinga uwepo wa Mungu (mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote) kwa sababu dhana ya kuwepo kwake ina contradiction.
The problem of evil poses a big contradiction for this God idea.
Naona unapenda vitabu, tena vitabu classic kama vya Plutarch. Mtu anayenitajia Plutarch mara moja namuangalia kama anafuatilia usomi.
Tuendeleze usomi, kujadiliana kwa usomi kunataka kusoma. Naomba tusome pamoja.
Naomba usome the attached book, kama hujakisoma, kinaitwa "The Philosophy of Religion: An Anthology", particularly see "PART IV The Problem of Evil page 276" in the attached book. If you haven't read and can read the entire book it will be even better, but the core of my critique is starting at "PART IV The Problem of Evil page 276"
Allah karimUnajua hata wewe unaweza kujiita mungu kama walivyofanya akina Beyonce na wengineo,mimi nafikiri tungejiuliza hasa ni nini maana ya Mungu?
Kwahiyo na Creator yupo mmoja au creator wa waislamu ni tofauti na wakristo na wa wakristo tofauti na wasio na creator wako wewe?hakuna mungu mmoja
wa kikristo ni tofauti na wa kihindi
wa kiislamu ni tofauti na wakichina
Kama unaamini sio spirit it's ok too sababu hata mimi sina uhakika, it is just a beliefUnajua wewe unachekesha sana nan alikuaminisha kuwa kuna creator ambaye ni spirit? ebu tuanzie hapo naona umahanyika tu
Uthibitisho haupo,hautaweza kuwepo sababu it never happened, wewe naweza kutumia falsafa zote kukuelewesha lakini hutoelewaWewe ndio sio muelewa,unachokiamini wewe ni tofauti na wanachoamini wenzako,wenzako wanaamini Mungu ila wewe hauamini Mungu unaamini tofauti na unasema Mungu ametungwa tu na watu,sasa wewe kama hauamini Mungu kuna haja gani ya kutaka kuthibitishiwa kitu kuhusiana na Mungu hali ya kuwa hauamini huyo Mungu?
Iwe kweli au sio kweli kuhusu kuongea na Mungu,wewe hilo suala linakushuglisha la nini hadi utake uthibitisho?
Nitaongea na wewe kwa mara ya mwisho, mimi ninapoclaim nimeongea na rais trump hiyo sio imani,ni kitendo ambacho inabidi nikithibitishe kuwa niliongea nae bila shaka(recorded convo,whateva), ninapoamini yupo rais anaitwa trump, hiyo inaweza kuwa imani na hatuna tatizo nayo, tatizo utakapoanza kusema trump kanimbia msiwe mnakula burger...itakubidi uthibitishe kauli yako.Hapo ndipo palipo na tatizo,unaposema mtu akiamini Allah huna tatizo naye wakati huyo Allah kabla ya kuaminiwa kwanza ameelezewa na watu ambao wamepata maelezo hayo kutoka kwa Allah mwenyewe na si kwamba wamejitungia tu wenyewe ila wewe ajabu unasema huna tatizo mtu akiamini Allah!
Unapinga watu kuongea na Mungu ila unakubaliana na watu hao hao wanapotoa maelezo kuhusu Mungu!