Ahsante kwa kunitajia Plutarch. Hivyo vitabu viwili vyote ninavyo na nimevisoma. Umenirudisha kuangalia kabati langu la vitabu vya historia ya enzi hizo.
Plutarch alikuwa mwanahistoria mzuri sana, hata Shakespeare alipoandika tamthiliya na michezo yake kuhusu Warumi, alimtumia Plutarch sana.
Tunaweza kusema Plutarch ni Shakespeare wa Shakespeare, kwa wasiomjua, lakini wanajua umuhimu wa Shakespeare, hilo linaweza kumuelezea umuhimu wake.
Lakini hilo halimfanyi Plutarch awe hawezi kukosea. Kuna mengi sana hakuyajua ambyao sisi tunayajua.
Habari ya kitu kujifanya chenyewe au kutojifanya chenyewe haithibitishi uwepo wa Mungu.
Kwa sababu, hata kama ulimwengu haiwezekani kuwa umejifanya wenyewe, hilo halimaanishi automatically kwamba umefanywa na Mungu.
Inawezekana ulimwengu haujajiumba wenyewe, na wala haujaumbwa na Mungu.
Na narudia tena, habari ya "kitu complex lazima kina aliyekifanya" inatuonesha Mungu hawezi kuwepo, kwa sababu Mungu naye ni complex na atahitaji muumbaji wake, na muumbaji wake atahitaji muumbaji wake, ad nauseum, ad infinitum.
View attachment 906505
Sijapinga uwepo wa Mungu kwa sababu haonekani, hagusiki, hanusiki etc.
Napinga uwepo wa Mungu (mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote) kwa sababu dhana ya kuwepo kwake ina contradiction.
The problem of evil poses a big contradiction for this God idea.
Naona unapenda vitabu, tena vitabu classic kama vya Plutarch. Mtu anayenitajia Plutarch mara moja namuangalia kama anafuatilia usomi.
Tuendeleze usomi, kujadiliana kwa usomi kunataka kusoma. Naomba tusome pamoja.
Naomba usome the attached book, kama hujakisoma, kinaitwa "The Philosophy of Religion: An Anthology", particularly see "PART IV The Problem of Evil page 276" in the attached book. If you haven't read and can read the entire book it will be even better, but the core of my critique is starting at "PART IV The Problem of Evil page 276"