PreGE2025 Godbless Lema acha mara moja kuingilia uhuru wa Vyombo vya Habari, huo udikteta uchwara uishie CHADEMA

PreGE2025 Godbless Lema acha mara moja kuingilia uhuru wa Vyombo vya Habari, huo udikteta uchwara uishie CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
View attachment 3295937

Watanzania wote tumepigwa na butwaa hii tabia mbaya ya kidikteta inayoota mizizi kwenye chama cha Chadema.
Baada ya kuwafunga midomo wanachama wa Chadema wasitoe maoni wala mawazo mbadala kwa kutishia kuwafukuza, kuwapa majina mabaya na kuwanyamazisha.

Sasa tunaona kiongozi wa Chadema mpya godbless Lema akijaribu kunyamazisha vyombo vya habari visitoe habari kuhusu kinachoendelea chadema.
Dunia nzima inajua chadema imepasuka vipande vikubwa viwili na watu wanataka kusikia kinachoendela.

Tunakataa huu udikteta unaoendelea ndani ya Chadema na wanataka kuuleta mpaka kwenye uhuru wa vyombo vya habari.

Godbless Lema nakuonya acha huu udikteta wenu ambao mnataka kutuletea kwenda hii nchi.
Usitusemee watanzania
 
Sema akili yako ndiyo iliyopasuka vipande viwili, siyo CHADEMA.

CHADEMA yenye wananchama milioni 10, kukatokea kakikundi ka watu hamsini kakajitenga na mamilioni ya wanachama, kwa upeo wako mdogo, utaita hayo ni makundi mawili? Hii inadhihirisha ni kiasi gani tasnia ya habari ya Tanzania imejengwa na watu wenye uwezo duni sana wa akili kiasi cha kushindwa kuchambua mambo kwa weledi!!
We hujui ht maana ya milioni 10, we huna tofauti na Heche anayesema kila siku wanajiunga wanachama mamilioni, nyie ni watu waliochanganyikiwa
 
Gazeti la Mwananchi unaona kabisa limepoteza Dira angalau lilikua gazeti linaandika vitu vinaeeleweka siku hizi ni G 55 kuanzia asbh mpaka kesho yaani linaandika vibaya upinzani kuliko hata gazeti la CCM la Uhuru.

Unaweza kusoma hilo gazeti ukashangaa inabidi wale watu wa chadema wawaandikie Agakhan wenyewe waone hilo genge liliko pale Tabata waliambie lifanye kazi kwa weledi.

Mwananchi ni hovyo kabisa kuliko Magazeti mengi hizi media za Tz zina ujinga sana
 
Kichwa cha habari na uhalisia ndani ya chama ni ardhi na mbingu.
Hivi ni nani ndani ya chama amelalamika kwamba ndani kuna mpasuko,
Mhariri hapo alichemka, na mimi namuunga mkono lema kwamba walitumika ama walipitiwa
 
Hao wahuni G55 njaa hawafiki popote ni genge jipya la CCM kujaribu kumdhoofisha Lissu na Heche.
 
Gazeti la Mwananchi unaona kabisa limepoteza Dira angalau lilikua gazeti linaandika vitu vinaeeleweka siku hizi ni G 55 kuanzia asbh mpaka kesho yaani linaandika vibaya upinzani kuliko hata gazeti la CCM la Uhuru.

Unaweza kusoma hilo gazeti ukashangaa inabidi wale watu wa chadema wawaandikie Agakhan wenyewe waone hilo genge liliko pale Tabata waliambie lifanye kazi kwa weledi.

Mwananchi ni hovyo kabisa kuliko Magazeti mengi hizi media za Tz zina ujinga sana
Udikteta mwisho Chadema. Vyombo vya habari tutavilinda kwa wivu mkubwa.
 
Back
Top Bottom