SI KWELI Godbless Lema amesema 'Tabia mojawapo mbaya ya masikini ni kuchukia matajiri'

SI KWELI Godbless Lema amesema 'Tabia mojawapo mbaya ya masikini ni kuchukia matajiri'

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
LEMA15SEP2025.jpg
 
Tunachokijua
Godbless Lema awali aliteuliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kabla ya uteuzi wake kutenguliwa na Msajili wa vyama vya siasa, na kisha baadaye kuteuliwa tena kwa ajili ya kukaimu nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Madai

Ipo taarifa inayosambazwa mtandaoni ikitumia utambulisho wa grafiki za Mwananchi na kunukuu ujumbe unaodaiwa kuchapishwa na Godbless Lema kuwa akisema 'Tabia mojawapo mbaya ya masikini ni kuchukia matajiri'

Uhalisia
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu yaani (Key Word Search) ulibaini kuwa ujumbe ulionukuliwa si halisi, bali ni wa kutengenezwa kwani haujachapishwa na Lema katika ukurasa wake kwenye mtandao wa X kama inavyoonekana.

Vilevile grafiki iliyotumika kusambaza taarifa hiyo, ni ya kughushi, kwani haijachapishwa na Mwananchi kama inavyoonekana bali wapotoshaji wametumia utambulisho huo kusambaza taarifa potofu.

Aidha kupitia ukurasa wake Lema ameikanusha taarifa hiyo na kwamba si ya kweli.​
He can't be imbecile like that. Uvisisiemu moron at their best, *** them.
 
Back
Top Bottom