- Source #1
- View Source #1
Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na machapisho mbalimbali yanayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Mojawapo ya machapisho hayo yanadai kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Godbless Lema, amesema kuwa kwa sasa anaonekana kama msaliti ndani ya chama.
Chapisho hilo, lililosambazwa kupitia Facebook, limenukuu kauli inayosema:"Asante Lema, usikubali kuchafuka kizembe wakati ukweli wa jambo unao wewe mwenyewe! Sema ukweli wote wa ufisadi wa Makamu Mwenyekiti Heche bila kuogopa, umma uko pamoja na wewe."
je, ni upi uhalisia wa chapisho hilo ambalo limeonekana kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii huku klikiwa na graphic ya chombo cha habari cha Jambo Tv ?

- Tunachokijua
- Godbless Lema ni mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA.
Karibuni kumekuwapo na madai ambayo yamekuwa yakimhusisha Lema kuwa amepokea fedha kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo kupitia mtandao wa X Lema alisisitiza kwa kusema
"Maazimio ya kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Kigoma yatatangazwa hivi karibuni na viongozi wakuu wa chama. Nina matumaini kwamba yatatoa majibu kwa kelele na mijadala mingi iliyoibuka hivi karibuni. Hata hivyo, iwapo italazimu kutetea heshima yangu binafsi dhidi ya kauli mbalimbali za dharau na upotoshaji, nitafanya hivyo kwa ufasaha. Nasikitika kwamba naweza kujikuta katika jaribu hilo, lakini heshima ya mtu si jambo la kupuuzwa."
Aidha kumekuwapo na chapisho linalosambazwa mtandaoni likiwa na kichwa cha habari kinachodai Lema amesema "Tunaonekana wasaliti ndani ya CHADEMA"
Je, ni upi uhalisia wa chapisho hilo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu yaani (Key Word Search) umebaini kuwa ujumbe ulionukuliwa si halisi, bali ni wa kutengenezwa na wapotoshaji kwani haujachapishwa na Lema katika ukurasa wake kwenye mtandao wa X kama inavyoonekana.
Vilevile grafiki iliyotumika kusambaza taarifa hiyo, ni ya kughushi, kwani haijachapishwa na Jambo TV, kama inavyoonekana bali wapotoshaji wametumia utambulisho huo kusambaza taarifa potofu.
Aidha grafiki iliyotumika muundo wake haufanani na machapisho rasmi kutoka kwenye chanzo hicho.