Pre GE2025 Godbless Lema: Ikiwezekana Mkutano Mkuu utoke na jina la mgombea Urais

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Siasa za chadema ni za kinafiki sana. Yeye Lema anasimama na nani kwenye huu uchaguzi?

Akiulizwa anasema watu wasubiri, anacheza mchezo wa hide and seek.
Atakayeshinda ndiye atakuwa wa kwake.
 
Lema analazimisha kumtafutia Lissu nafasi ya kugombea urais ikiwa atashindwa uenyekiti.

Wazo hili la Lema halitolewi kwa nia njema.

Mafahali wawili hawakai zizi moja . Lissu lazima afukuzwe.

Je ikitokea huko mbeleni kuna mgombea maarufu zaidii akaibuka na kuonekana anafaa zaidi kugombea urais wa,kati tayari chama kimeishateua mgombea, Lema haoni hiyo itakuathiri chama kupata mgombea bora?
 
Sitaki kuamini kama wajumbe mkutano mkuu woote ni wajinga kwa kutuletea tena Mbowe, wanaweza kuwemo wajinga ila wachache jamaa king'ang'anizi aambulie kura japo % 2 tuu kudadek zake!!.
Ni kweli wajumbe sio wajinga ila tambua hao wajumbe wamekijenga chama wakiwa na Mbowe na wengine wana zaidi ya miaka 20 wakiwa wajumbe.
 
hiyo itakua ni kuminya haki na fursa kwa wanachadema wasio wajumbe wa mkutano mkuu, wenye nia na malengo ya kugombea urasi 2025, ambao wanaosubiri utaratibu wa kichama utangazwe na kupitia hatua zote za kikatiba kutimiza azma zao za kisiasa.

Ni muhimu wazo la lema likaheshimiwa lakini likapuuzwa 🐒
 
Kwenye demokrasia ili uweze kufanikisha kitu kuna wakati mpaka wa katiba huwa unasogezwa kidogo.

Mfano huwa wanasema kila mtu ana uhuru wa kuongea, badae utasikia lkn sio ndani ya kuta za ikulu.
 
Kwani lini mmebadili msimamo? Si mlisema hamtashiriki hadi Katiba Mpya.Basi sawa,ngoja CCM tujipange kuwashughulikia.
 
Kamati kuu ipi? Hii inayomaliza muda wake? Hii itakuwa sio sawa, kamati kuu mpya na secretariet mpya ishughulike na mambo hayo
 
Hizi ni mbinu za kuwapooza timu Lissu Ili wasiondoke Chadema pale watakapopokwa uenyekiti....

Lissu usikubali hii rushwa.
 
Katiba ya CDM inasemaje kuhusu namna ya kumpata mgombea urais?
 
Lema naye kachoka kisiasa
Yeye alisema no reform no election za sasa anaongelea uteuzi wa wagombea

Ukiwa muongo usiwe msahaulifu
Kwani kuteua mgombea ndio kugombea!!??
Watu mnaakili ndogo sana.
 
CDM Wanatakiwa kutuonyesha mfano wa jinsi ya kuendesha mambo kidemkrasia. Atakayeshinda aachwe aongoze chama iwe FAM au TAL. Haya makolokolo mengine yanayoendelea ndani ya chama hayahusiani na Demokrasia.
 
Lissu mwenyekiti, Lemma makamu mwenyekiti na Heche Katibu mkuu. Mgombea urais Lissu.
Wachaga huwa hawasalitiani pia watu wa kaskazini mashariki hawasalitiani. Ni rahisi kupigana wao kwa wao lakini akija mtu nje ya wao wanaungana wanampiga kimyakimya au kwa uwazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…