Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Ndugu Lema, nakusabahi
Miaka michache iliyopita, wakati ukiwa Canada, na Lissu akiwa ubelgiji mlikuwa mkitoa elimu nzito kuhusu demokrasia na mambo ya uchaguzi. Miongoni mwq elimu nzito mlizokuwa mkitoa ni kuwa, haiwezekani uchaguzi nchini ukawa huru na wa haki kwa katiba na sheria hizi. Kwa kweli elimu ilifika, watanzania wakawaelewa. Wengi wakaacha kushiriki hata chaguzi za marudio kwa sababu waliona kuwa mnachoongea kina logic.
Lakini hamkuishia hapo, wewe binafsi ulisema unachopigania siyo madaraka, wala ubunge bali mustakbali mwema wa Taifa, na umewahi kupendekeza kuwa Rais Samia hata akiamua kupitisha miaka mitano asiitishe uchaguzi ilimradi afanyie kazi ishu ya katiba mpya, kwako hiyo ni sawa tu.
Ndugu Lissu yeye akatumia utaalamu wake wa kisheria kuelimisha watu mapungufu mazito ya sheria tulizonazo kuhusiana na chaguzi. Ndugu Lissu akasema, Ni UJINGA kushiriki chaguzi chini ya katiba hii na sheria hizi. Kwa kweli elimu yake ilifika kwa wananchi ipasavyo.
Ukiachilia mbali hivyo, Mwenyekiti wa chama chenu ndugu Mbowe, mara baada ya uchaguzi wa 2020 alisoma azimio akasema kuwa CHADEMA haitoshiriki chaguzi kwa katiba hii na sheria hizi maana uchaguzi hauwezi kuwa huru na haki.
Sasa ndugu Lema, lini mmegeuka Paulo akiwa njiani kuelekea Damascus, kwa kuona kuwa upo uwezekano wa uchaguzi chini ya katiba hii kuwa na maana?
Maana ndugu Lema, kuwaambia wananchi wakashiriki uchaguzi hata kama kuna figisu ili tuweze kujua kuwa CCM imeiba kura haitoshi. Sasa tukishajua then WHAT?
Na pia tkienda kushiriki chaguzi kwa katiba na sheria hizi mbovu kuoita kiasi kimsingi mnakuwa mnatafuta uhai wa chama zaidi kuliko kusaidia taifa kurekebisha mambo.
SOLUTION
1. Msimamo wa mwanzo wa chama ndiyo sahihi, Kupigania katiba mpya mpaka kieleweke. Kushiriki chaguzi wakati wewe unajua, wananchi wanajua kuwa CCM itachakachua ni kuihalalishia CCM katika uchakachuaji kwa kuwapa ushiriki.
2. Umma uendelee kuandaliwa kuidharau na kuipuuza CCM ktk mambo yake
3. Zitafutwe njia na mbinu halali za migomo mbalimbali za kuipiga presha serikali ya CCM ikae mezani na kufanya reforms za msingi
Naungana na Lissu wa mwaka 2020-2022 kuwa kushiriki chaguzi ktk hali hii tuliyonayo ni UJINGA