Mkuu 'Missile', na wasomaji na wachangiaji wa mada yako hii muhimu, binafsi sioni sababu ya kuwalaumu akina Lemma, Lissu na viongozi wengine wa CHADEMA kwa hayo uliyo yaeleza kwenye mada yako.
Hayo uliyo yataja ya "Kutoshiriki uchaguzi bila uwepo wa Katiba Mpya na Tume Huru", yalisemwa mwanzoni kabisa baada ya uchafuzi ule uliofanyika 2020, na baada ya mchafuzi mkuu kuondoka kwenye picha. Matarajio ya wakati huo, na uwepo wa muda wa kutosha kufanya marekebisho hayo ulikuwepo. Huyo kiongozi mpya aliyeingia na kushika nafasi, naye alionyesha dalili za mwelekeo wa hayo kufanyika.
Kwa hiyo, kabla ya kuyang'ang'ania hayo kuwa sababu ya kulaumu na kuanza kuhimiza watu wasipige kura ni muhimu kuyapima vizuri kwenye mizani.
Ni lini hasa kauli ya kususia uchaguzi endapo hapatakuwepo na Katiba Mpya na Tume huru iligeuzwa na viongozi hawa na chama chao?
Mimi nadhani ni baada ya kubainika wazi kwamba Samia katekwa na wahafidhina ndani ya CCM. Akatupilia mbali ule ulaghai wa mazungumzo ya maridhiano; wakati akisha mteka nyara Mbowe! Baada ya hapo, habari ya ufinyu wa muda unaotakiwa kutengeneza Katiba Mpya ukawa ni kizingiti. Tume Huru wakaona urahisi wa kutengeneza mazingaombwe, kama walivyo fanya.
Nirudi nyuma kidogo: baadhi yetu toka mwanzo kabisa tulikuwa tukiwahimiza CHADEMA kwamba kama hapatakuwepo na mabadiliko ya Katiba na uwepo wa tume huru, CHADEMA na wengine wajiandae KUZUIA UCHAGUZI kwa njia yoyote ile iwezekanayo, na siyo kususia tu uchaguzi.
Sasa tumefika hapa, Oktoba, tayari CCM ikijiandaa kufanya yale yale ya siku zote, tena waziwazi kabisa bila ya kificho.
CHADEMA wasusie uchaguzi. Itasaidia kitu gani? CCM itatakaza matokeo tena siyo ya namba ya waliowapa kura; watatangaza Asili mia ya ushindi walio upata; bila shaka si chini ya asili mia 90!
Kususia uchaguzi kutakuwa kumesaidia kitu gani!
Hebu tutazame huo upande wa ;pili; ambao wanawahimiza wananchi wajiandikishe kwa wingi zaidi na wajitokeze kupiga kura kuliko wakati mwingine wowote.
Tukikubaliana kuwa hawa watakao pata hamasa ya kujiandikisha na kupiga kura watakuwa ni wanaotaka mabadiliko, ni kuwa kura hizo nyingi zitakuwa ni za kuwakataa CCM
Sasa hapa litakuwa jukumu la CCM kuzikataa/kuzificha hizi kura nyingi zilizo wakataa. Hiyo moja.
Pili, lengo la ushauri wetu kwa CHADEMA kuwahimiza wananchi wengi kushiriki, ni kuwa wananchi hawa watakuwa wamepata elimu ya kutosha kuhusu HAKI zao na uhalali wa kura zao walizo piga. Kwamba wananchi hawa waandaliwe kukataa uvunjwaji wa sheria unaofanywa na CCM, huko huko kwenye vituo vyao vya kupigia kura na kuhesabu na kutangaza kura hizo. CHADEMA na vyama vingine wanao wananchi na wanachama wao karibu kila mahala nchini, kwa hiyo kituo chochote cha kupigia kura nchi nzima pasinge wezekana kukosa wananchi wa kukataa kura zao zisiharibiwe, huko huko kwenye vituo na kwenye ngazi nyinginezo katika hatua za kutangaza matokeo.
Bahati mbaya sana ninayo walaumu viongozi wa CHADEMA, kazi ya maandalizi ya wananchi kufanya kazi hii iliwashinda toka mwanzo. Sijui kwa kweli kilicho tokea ndani ya chama hiki kilicho anza kuweka matumaini kwa wananchi.
Nime tiririka tu, bila mpangilio maalum, lakini ni matumaini yangu kwamba nitaeleweka ukinifuatilia vizuri nilicho jaribu kueleza hapa.
Mkuu, 'Missile' naheshimu sana mada zako unazoleta hapa jamvini. Ni mada ulizo ziandaa na kuzipa wakati wa kutosha kuzipangilia vizuri.