Pre GE2025 Godbless Lema: Uchaguzi 'huru na haki', umeongeza heshima kwa Mbowe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sikuamini kama tutavuka salama huu uchaguzi.. Niliteseka mno kila nikiona ile mitifuano ya makada
Kuna siku nili quote mchango wako humu nikaeleza hofu yangu.Actually nilikuwa nimekata tamaa.Hofu yangu kubwa ilikuwa kwenye yale yatakayotokea iwapo kusingekuwa na transparency kama iliyokuwepo.Walau sasa tunayo reference ya nini maana ya uchaguzi huru na haki.Asanteni CHADEMA
 
Atleast sasa Mbowe hatonenewa mabaya tena kama ambavyo ilikua kwenye kampeni.
Mbowe anastahili heshima kubwa sanaa Nchi hii. Mapumziko mema Mzee wetu
 
Mmemtukana sana naye amekuwa humble; kila uzushi Mbowe alizushiwa kuanzia kula ruzuku yote makao makuu bila kupeleka majimboni, rushwa, kuuza chama, kutopata hata mbunge na diwani hata mmoja 2020 wakati wote mnajua hakukuwa na uchaguzi mkuu bali uchafuzi.

Muda ni mwalimu mzuri, tunasubiri tuone mtafanya miujiza gani ili hiyo ruzuku kidogo ya sh milioni mia itumike kuendesha makao makuu, operesheni zake nchi nzima na ibakie ya kupeleka katika majimbo; mje mtupe update mmepeleka ngapi majimbo yote . Pia uchaguzi ujao tuone namba ya wabunge na madiwani mtakaopata.

Tunasubiri utekelezaji wa no reform no election ili tuone kama kweli mtaweza kusimamisha uchaguzi mkuu usifanyike maana nina hakika reforms haitafanyika.

Kila la heri uongozi mpya.

Mwana kulitafuta mwana kulipata.
 
Wewe ndiye utakipasua mkuu? Umepanga kukipasua lini? Hata akina Nchimbi walimuunga mkono Lowasa lakini leo hii anatarajiwa kuwa makamu wa Rais ikiwa CCM itashinda. CHADEMA hakuna mgogoro mkuu.
mbowe kaweka heshima? subiri uone chama kinavyopasuka
 
Huyu ni Nunda mla watu, wala Mbowe usimwamini. Kuna kitu wanataka kufany: KUKUSIFIA KWA MBWEMBWE NYINGI! TAKE CARE ili usahau
 
mulimtukana Sana mBowe saivi wanafanya unafiki. Ila CHADEMA ya Lissu kikishndiwa kuchukua nchi 2025 wataaibika sana
 
Mbowe alilaumiwa sana

sasa na wao wapeleke chama mbele zaidi na chaguzi zijazo wasing'ang'anie madaraka wakishindwa wapishe bila kinyongo wala kuchakachua uchaguzi
 

..jamani tutumie neno TANGANYIKA, tuachane na Tanzania Bara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…