Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema, amesema wakati maandamano yakiendelea Oktoba 29, Boni Yai pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Amani Golugwa, walimpigia simu na kumueleza kuwa watu kutoka Ikulu walikuwa wanataka kuzungumza na viongozi wa Chadema ili kusaidia kupunguza maandamano yaliyokuwa yanaendelea katika baadhi ya maeneo nchini.
Soma Pia: Video: Kimara wameshaanza kutesti mitambo. Watu wameanza kuingia barabarani
“Boni Yai ananipigia simu pamoja na Naibu Katibu Mkuu siku ya pili, wakaniambia ‘upo wapi?’ Nikasema nipo Arusha. Wakauliza, ‘Arusha hali ikoje?’ Nikawajibu naogopa hata kutoka nje. Akasema watu wa Ikulu wamepiga simu wanaomba Chadema isaidie kutuliza maandamano. Wanataka tukutane. Mimi sina shida ya kukutana na hao watu, hata chama chetu mkiniuliza nitasema kutaneni nao, wakati huo Makamu wetu yupo jela na Mwenyekiti yupo jela,” amesema Godbless Lema.