Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Godfrey Sitta, mtia nia wa Ubunge wa jimbo la Meatu kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) ametoa wito kwa makada wa chama hicho na wakazi wa Meatu kwa ujumla wake kuhakikisha wanaufanyia kazi kikamilifu ushauri uliotolewa na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara ya kikazi hivi karibuni mkoani Simiyu.
Godfrey Sitta amesema Rais Samia Suluhu Hassan alitoa wito kwa wakazi wa Meatu na mkoa wa Simiyu kwa ujumla wake kuhakikisha wanachagua viongozi watakaokuwa tayari kuwapigania kuwaletea maendeleo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Kada huyo wa CCM amesema amelazimika kutoa ukumbusho huo kutokana na kile alichodai kuwa uwepo wa viashiria vya rushwa kwa baadhi ya watia nia wenzake, hali inayotilia shaka weledi wa Kamati ya siasa ya wilaya iliyohusika kufanya mapendekezo ya awali ya watia nia hayo, akidai kuwa baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wana maslahi binafsi na baadhi ya watia nia.