Godlisten Malisa: Ili tuweze kusafirisha umeme sisi wenyewe kwa tija inabidi tujenge vituo vya kupozea njiani

Irene17

New Member
Joined
Feb 8, 2025
Posts
3
Reaction score
23
By Malisa GJ,

Kwanza, ieleweke kuwa hili si jambo geni. Hii si mara ya kwanza kununua umeme nje ya nchi. Tunanunua umeme kutoka Zambia kwa ajili ya mkoa wa Rukwa, kutoka Uganda kwa ajili ya mkoa wa Kagera, na kutoka Kenya kwa ajili ya wilaya ya Mkinga, Tanga.

Pili, watanzania tunahoji kwanini tununue umeme nje wakati tuliambiwa bwawa la Nyerere likikamilika tutakuwa na umeme wa kutosha na tutaweza kuuza nje. Je, tulidanganywa?

Ili kujibu swali hilo ni muhimu kujua hali ya uzalishaji wa umeme nchini na vyanzo vyake. Vyanzo vya umeme wa maji (hydroelectric power plants) tulivyonavyo vina uwezo ufuatao:
  • Kidatu inazalisha 204 MW
  • Kihansi 180 MW
  • Mtera 80 MW
  • Hale (Tanga) 68 MW
  • Rusumo 80 MW
  • Julius Nyerere 2,115 MW
  • Nyumba ya Mungu 8 MW

Kwa hiyo, kupitia vyanzo vya maji tuna uwezo wa kuzalisha 2,735 MW. Mahitaji ya umeme nchini yanakadiriwa kuwa 2,200 MW. Hii ina maana kwamba tuna ziada ya karibu 500 MW ambazo tunaweza kuuza nje. Kwa hiyo hatujadanganywa. Umeme wa kuuza nje upo.

Sasa, kwanini tununue umeme nje wakati ndani tuna ziada? Jibu ni kwamba usafirishaji wa umeme unasababisha upotevu njiani. Kusafirisha umeme si sawa na kusafirisha mbaazi. Ukitoa mbaazi Moshi zikiwa 50Kgs, zikifika Dar zitakua hizohizo 50Kgs. Lakini kwa Umeme ni tofauti. Kadri unavyosafirisha umbali mrefu, ndivyo unavyopotea.

Je, kati ya Ethiopia na bwawa la Mwalimu Nyerere, wapi mbali? Kama tunahofia umeme ukisafirishwa kutoka bwawa la Nyerere hadi Arusha utapotea, je unaotoka Ethiopia si utapotea zaidi?

Jibu ni kwamba Tanzania haitahusika na usafirishaji wa umeme huo kutoka Ethiopia. Sisi tutahusika baada ya kuupokea Namanga. Kwa hiyo, kama ni usafirishaji, sisi tutaanzia Namanga kwenda Arusha. Kwahiyo pale Namanga tukipokea 100MWs tutazifikisha Arusha bila kupotea maana ni karibu.

Kwa lugha rahisi, ni sawa na kuwa na chanzo kipya cha umeme Namanga. Kwa hiyo ni ukweli kwamba kusafirisha umeme kutoka Namanga kwenda Arusha hakutakuwa na upotevu mkubwa njiani kama kusafirisha umeme kutoka bwawa la Nyerere kwenda Arusha. Hii ni logic ya kawaida ambayo hata mtoto mdogo anaelewa.

Soma Pia: Rais Samia: Serikali itanunua Umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini

Ili tuweze kusafirisha umeme kutoka bwawa la Nyerere au Mtera hadi Arusha bila kupotea sana, inabidi tujenge vituo vya kupoozea njiani (substations) kama ile ya Lemuguru iliyopo Mateves Arusha, ambayo ilianza kujengwa 2019 imekamilika 2024 (miaka mitano) kwa gharama ya karibu bilioni 20. Kwa hiyo kuna suala la muda na gharama.

Je, umeme wa ziada unaozalishwa Tanzania utaenda wapi? Jibu ni kwamba Utauzwa nje ya nchi. Tayari Tanzania imesaini hati ya makubaliano (MoU) na Zambia na Rwanda kuziuzia umeme.

Je, kusafirisha umeme kwenda nchi hizo hakutafanya upotee njiani? Jibu ni kwamba umeme huo utauzwa kutoka vyanzo vya karibu, hivyo hakutakuwa na upotevu mkubwa. Kwa mfano, Rwanda watauziwa umeme kutoka Rusumo na Zambia watapokea umeme kutoka Kihansi ambapo upotevu hauwezi kuwa mkubwa kama kuutoa umeme Kihansi kwenda Arusha au Rusumo kwenda Arusha.

Utaratibu wa kuuziana umeme baina ya nchi na nchi sio jambo geni. Nchi za Afrika Mashariki zimeanzisha Eastern Africa Power Pool (EAPP) ili kuratibu biashara ya umeme na uunganishaji wa gridi kati ya nchi hizo.

Nchi za Ulaya wanayo European Network of Transmission System Operators for Electricity (ENTSO-E) ambayo inaunganisha nchi 35 za Ulaya. Kupitia ENTSO-E nchi inaweza kuuza na kununua umeme kutoka nchi jirani. Kwa mfano, Ujerumani inanunua umeme kutoka Ufaransa, Denmark, na Norway jumla ya 30,000 MW. Lakini Ujerumani hiyohiyo inauza umeme kwa Ufaransa, Austria, na Uholanzi ambao ni 60,000 MW.

Unaweza kujiuliza, kama Ujerumani inaweza kuzalisha umeme na kuuza nje ya nchi, kwanini tena inunue? Jibu ni kwamba inapunguza upotevu wa kusafirisha umeme kwa umbali mrefu ndani ya nchi. Kuliko kutoa umeme Munich na kuusafirisha hadi Humburg (kilomita karibu 800) ni bora wakanunua umeme Dernmark wakapeleka Humburg, halafu ule wanaozalisha Munich ukatumika miji ya jirani na mwingine wakauzia Austria.

Na Tanzania ndicho tulichofanya. Kuliko kutoa umeme Rusumo kuupeleka Kyela, ni bora ule wa Rusumo utumike Kigoma, Kagera, na Geita, halafu unaobaki tuwauzie Rwanda na Burundi. Halafu tununue umeme kutoka Malawi tupeleke Kyela. Tukifanya hivyo tutakua tumeokoa gharama za usafirishaji na upotevu wa umeme njiani.!
 
Elimu nzuri kabisa ya umeme.
P
 
Umeme huo ni kwa ajili ya kaskazini, Cleopa alikuwepo hakuliona, Mramba hakuliona Hilo, Wataalamu wetu hawajaliona Hilo. Maria ndio ameliona Hilo
 
Ukisoma paragraph mbili za mwanzo tu ukakimbilia ku comment waweza kumuita Malisa majina yote ya ajabu.., chawa, kanunuliwa etc, lakini ukisoma mpaka mwisho utaishia kumpa like, tatizo ufafanuzi wa serikali haupo kitaalam. Na mtu wa kwanza kutangazia taifa kuhusu hili pengine naye hana uelewa wa haya yaliyopo kwenye hii thread... Ila poa tu, twende hivyohivyo.
 
By Malisa GJ,

Kwanza, ieleweke kuwa hili si jambo geni. Hii si mara ya kwanza kununua umeme nje ya nchi. Tunanunua umeme kutoka Zambia kwa ajili ya mkoa wa Rukwa, kutoka Uganda kwa ajili ya mkoa wa Kagera, na kutoka Kenya kwa ajili ya wilaya ya Mkinga, Tanga.

Pili, watanzania tunahoji kwanini tununue umeme nje wakati tuliambiwa bwawa la Nyerere likikamilika tutakuwa na umeme wa kutosha na tutaweza kuuza nje. Je, tulidanganywa?

Ili kujibu swali hilo ni muhimu kujua hali ya uzalishaji wa umeme nchini na vyanzo vyake. Vyanzo vya umeme wa maji (hydroelectric power plants) tulivyonavyo vina uwezo ufuatao:
  • Kidatu inazalisha 204 MW
  • Kihansi 180 MW
  • Mtera 80 MW
  • Hale (Tanga) 68 MW
  • Rusumo 80 MW
  • Julius Nyerere 2,115 MW
  • Nyumba ya Mungu 8 MW

Kwa hiyo, kupitia vyanzo vya maji tuna uwezo wa kuzalisha 2,735 MW. Mahitaji ya umeme nchini yanakadiriwa kuwa 2,200 MW. Hii ina maana kwamba tuna ziada ya karibu 500 MW ambazo tunaweza kuuza nje. Kwa hiyo hatujadanganywa. Umeme wa kuuza nje upo.

Sasa, kwanini tununue umeme nje wakati ndani tuna ziada? Jibu ni kwamba usafirishaji wa umeme unasababisha upotevu njiani. Kusafirisha umeme si sawa na kusafirisha mbaazi. Ukitoa mbaazi Moshi zikiwa 50Kgs, zikifika Dar zitakua hizohizo 50Kgs. Lakini kwa Umeme ni tofauti. Kadri unavyosafirisha umbali mrefu, ndivyo unavyopotea.

Je, kati ya Ethiopia na bwawa la Mwalimu Nyerere, wapi mbali? Kama tunahofia umeme ukisafirishwa kutoka bwawa la Nyerere hadi Arusha utapotea, je unaotoka Ethiopia si utapotea zaidi?

Jibu ni kwamba Tanzania haitahusika na usafirishaji wa umeme huo kutoka Ethiopia. Sisi tutahusika baada ya kuupokea Namanga. Kwa hiyo, kama ni usafirishaji, sisi tutaanzia Namanga kwenda Arusha. Kwahiyo pale Namanga tukipokea 100MWs tutazifikisha Arusha bila kupotea maana ni karibu.

Kwa lugha rahisi, ni sawa na kuwa na chanzo kipya cha umeme Namanga. Kwa hiyo ni ukweli kwamba kusafirisha umeme kutoka Namanga kwenda Arusha hakutakuwa na upotevu mkubwa njiani kama kusafirisha umeme kutoka bwawa la Nyerere kwenda Arusha. Hii ni logic ya kawaida ambayo hata mtoto mdogo anaelewa.

Soma Pia: Rais Samia: Serikali itanunua Umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini

Ili tuweze kusafirisha umeme kutoka bwawa la Nyerere au Mtera hadi Arusha bila kupotea sana, inabidi tujenge vituo vya kupoozea njiani (substations) kama ile ya Lemuguru iliyopo Mateves Arusha, ambayo ilianza kujengwa 2019 imekamilika 2024 (miaka mitano) kwa gharama ya karibu bilioni 20. Kwa hiyo kuna suala la muda na gharama.

Je, umeme wa ziada unaozalishwa Tanzania utaenda wapi? Jibu ni kwamba Utauzwa nje ya nchi. Tayari Tanzania imesaini hati ya makubaliano (MoU) na Zambia na Rwanda kuziuzia umeme.

Je, kusafirisha umeme kwenda nchi hizo hakutafanya upotee njiani? Jibu ni kwamba umeme huo utauzwa kutoka vyanzo vya karibu, hivyo hakutakuwa na upotevu mkubwa. Kwa mfano, Rwanda watauziwa umeme kutoka Rusumo na Zambia watapokea umeme kutoka Kihansi ambapo upotevu hauwezi kuwa mkubwa kama kuutoa umeme Kihansi kwenda Arusha au Rusumo kwenda Arusha.

Utaratibu wa kuuziana umeme baina ya nchi na nchi sio jambo geni. Nchi za Afrika Mashariki zimeanzisha Eastern Africa Power Pool (EAPP) ili kuratibu biashara ya umeme na uunganishaji wa gridi kati ya nchi hizo.

Nchi za Ulaya wanayo European Network of Transmission System Operators for Electricity (ENTSO-E) ambayo inaunganisha nchi 35 za Ulaya. Kupitia ENTSO-E nchi inaweza kuuza na kununua umeme kutoka nchi jirani. Kwa mfano, Ujerumani inanunua umeme kutoka Ufaransa, Denmark, na Norway jumla ya 30,000 MW. Lakini Ujerumani hiyohiyo inauza umeme kwa Ufaransa, Austria, na Uholanzi ambao ni 60,000 MW.

Unaweza kujiuliza, kama Ujerumani inaweza kuzalisha umeme na kuuza nje ya nchi, kwanini tena inunue? Jibu ni kwamba inapunguza upotevu wa kusafirisha umeme kwa umbali mrefu ndani ya nchi. Kuliko kutoa umeme Munich na kuusafirisha hadi Humburg (kilomita karibu 800) ni bora wakanunua umeme Dernmark wakapeleka Humburg, halafu ule wanaozalisha Munich ukatumika miji ya jirani na mwingine wakauzia Austria.

Na Tanzania ndicho tulichofanya. Kuliko kutoa umeme Rusumo kuupeleka Kyela, ni bora ule wa Rusumo utumike Kigoma, Kagera, na Geita, halafu unaobaki tuwauzie Rwanda na Burundi. Halafu tununue umeme kutoka Malawi tupeleke Kyela. Tukifanya hivyo tutakua tumeokoa gharama za usafirishaji na upotevu wa umeme njiani.!
Umeelezea vzr sana mtaalam, umenitoa tongotongo sana
 
na hivyo vyanzo vyote vilijengwa na Nyerere, Mkapa na Magufuli na wote watatu had one thing in common, walikuwa ni Christians
 
siyo kweli, Ujerumani inanunua umeme nje kwa sababu haina umeme wa kutosha, jiulizeni nchi zenye umeme wa kutosha kama France kama zinanunua umeme nje, bottom line wanaonunua umeme nje hawazalishi umeme wa kutosha, maelezo marefu lkn yamejaa uongo na upotoshaji, huo umeme wanaotaka kununua unatokea ethiopia, unavuka nchi nzima ya kenya ndiyo ufike kwetu, hilo limewezekana vipi?

acheni kupotosha ujerumani ilifunga na kuzima umeme wake wa nuclear ndiyo maana wana import kwa kuwa hawana umeme wa kutosha …
 
Elimu nzuri kabisa ya umeme.
P

imejaa uongo na upotoshaji, wanao import umeme wote wanafanya hivyo kwa sababu hawazalishi umeme wa kutosha ndani ya nchi yao, period. isitoshe huo umeme tanzagiza hawanunui ktk kenya bali unatokea ethiopia, sasa ethiopia waliwezaje kuusafirisha umeme kupita nchi nzima ya kenya mpaka ufike kwetu? sisi hatuma mpaka na ethiopia, je upotevu wa umeme haupo hapo?

na vipi khs gharama? tutawalipa kenya na ethiopia kwa kutuuzia umeme kwani kenya siyo umeme wao lkn umepitia kwao hivyo tunalipia gharama za miundo mbinu walizotumia kuvuta umeme ktk ethiopia mpaka kenya, kwa kifupi tumechangia gharama za ujenzi na uendeshaji wa the Grand Renaissance Dam -ethiopia.

the country is being mismanaged and destroyed to the ground …
 
Wana JF, nilikua najaribu kuwaza, hivi kama Tz inazalisha umeme lakini hauna manufaa kuupeleka Kasikazini kwasababu ni mbali na kuamua kununua wa Ethopia, Je umeme tunaotaka kuwauzia majirani zetu kama Zambia, Malawi, Kenya na wengine utafikaje huko?

Nisaidieni kupata majibu.
 
We jua tu watu wanatengeneza mlija mpya wa pesa, waendlee kula mema ya nchi.

OVA
 
Kaskazini wajitafakari sana kama wao ni sehemu ya Tanzania.
Kama Serikali ya Dodoma imewachoka watu wa Kaskazini wawaruhusu wajiunge na Kenya na Uganda
 
Wana JF, nilikua najaribu kuwaza, hivi kama Tz inazalisha umeme lakini hauna manufaa kuupeleka Kasikazini kwasababu ni mbali na kuamua kununua wa Ethopia, Je umeme tunaotaka kuwauzia majirani zetu kama Zambia, Malawi, Kenya na wengine utafikaje huko?

Nisaidieni kupata majibu.
Comment ya kwanza kakudanganya, ila nikueleze serikali ilishatoa maelezo nadhani hufatilii.
Tanzania ni mwanachama wa
southern africa power
Eastern Africa power
Kuna miundombinu ya moja kwa moja kama kenya tz interconnect na ule tz zambia interconnect.
Tanzania ina njia kuu zinazotoka iringa, shinyanga na mbeya, ambazo zinaunganishwa na njia za kimataifa, ili kusafirisha kwa wenzetu majirani,
Ila nikuibie siri baada ya yote. Tanzania ipo kwenye mradi wa backbone transmission line.
 
Hii ni plan ya Utapeli wa watu wachache ambao ni very powerful kwenye system, huenda Mama kizimkazi anaogopa kilicho mkuta new boss,
 
Back
Top Bottom