Godlisten Malisa: Ili tuweze kusafirisha umeme sisi wenyewe kwa tija inabidi tujenge vituo vya kupozea njiani

Kwamba Tanzania itachukua umeme kuanzia Namanga. Je, Hapo Namanga huo umeme umefikaje kutoka Ethiopia? Ni nani atalipa hizo gharama za kuutoa kutoka Ethiopia hadi Namanga ili Tanzania ije ijichukulie kirahisi hivyo?
 
Kwa hiyo principles za ugavi wa umeme na uchumi ni unique kwa Tz tu? If X doesn't work in country A why would X work just fine in country B? Help us understand this
 
Chako ni chako
Bora tugharamie umeme wetu kuliko kutegemea kwa jirani, je ikatokea Misri wakaipiga Ethiopia mikoa ya KAT tutaponea wapi
 
Hapa huyu anatetea kitu kinachoenda kanda yao, ingekuwa kinaenda kanda tofauti angekuja na all sort of analysis kuonesha mradi wa kununua nje haufai. Nilishangaa sana kipindi cha nyuma kila miradi ilikuwa inapopolewa ati ni maendeleo ya vitu na si ya watu. Ila daraja la mto wami ule mradi haukupopolewa, guess why?
 
Nimekuelewa vizuri mkuu, huwa wana asili ya u selfish..
 
Tumekatiwa sana umeme kwa kisingizio cha maboresho ya miundombinu ya Gridi kumbe ilikuwa ni sound tu
 
Tuache siasa pembeni, hili suala linajulikana toka tulipoanza hii miradi ya kuzalisha umeme na usafirishaji wake, na hivyo hivyo nategemea vituo vya kupozea umeme vilishapangwa. Sasa ni vizuri tukafuata Mipango mikakati yetu hata kama itachuku muda lakini ndo Hali yetu
 
Chako ni chako
Bora tugharamie umeme wetu kuliko kutegemea kwa jirani, je ikatokea Misri wakaipiga Ethiopia mikoa ya KAT tutaponea wapi
Sahv kuna mkakati nchi za africa wanataka ku link umeme pamoja
Usije shanga kusikia umeme wetu ukaenda mpk afrika kusini

Ova
 
Mimi swali langu ni hili.

Je ili sisi tuuze tutalazimika kuusafirisha kutoka Rufiji mpaka Mpakani? Je wa kwetu tukisafirisha mpaka mpakani hautapotea?

Au wao wataninua umeme rufiji sio kama sisi tutakavyo nunua Mpakani?
 
Je ili sisi tuuze tutalazimika kuusafirisha kutoka Rufiji mpaka Mpakani? Je wa kwetu tukisafirisha mpaka mpakani hautapotea?
Portential customer ni huyo dogo hapo ng'ambo aliyesema anaweza kurejea kwenye vibatari aliposhindwa kulipa bills
 
Kihansi -Arusha na Kihansi-Zambia wapi karibu?
Jengeni vipoza umeme na njia mpya zenye ubora,acheni longolongo
 

PINGAMIZI DHIDI YA HOJA YA MALISA ANAYETETEA TABIA YA SERIKALI YA TANZANIA KUTEMBEZA BAKULI LA KUOMBA UMEME UGHAIBUNI: HATUDANGANYIKI


Waziri Mkuu Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko

Katika pingamizi hili napendekeza kwamba, kadiri jukumu la kuzalisha na kusambaza umeme kwa kutumia tekinolojia ya kisasa linavyohusika, uamuzi wa serikali ya Tanzania kuhemea umeme kutoka ughaibuni, hapa katika zama za "post-Stigler's Gorge," ni ushahidi tosha kwamba serikali haikutekeleza wajibu wake ipasavyo kwa wakati, na sasa inahaha kuokoa jahazi.

Kimsingi, maelezo ya Malisa kuhusu nishati ya umeme yamenikumbusha Mwalimu wangu wa Fizikia, Dr. Kiwanga, Idara ya Fizikia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Alinifundisha Kanuni ya Ohm kuhusu usafirishaji wa umeme, yaani Ohms Law. Kanuni hii inasema kwamba:

(1) V=IR;

(2) R=(r*L)/A;

(3) I=(V/R) kutokana na (1);

(4) P=V*I

(5) P=I*I*R Kutokana na (1) na (4);

(6) P= (I*I*r*L)/A kutokana na (2) na (5);

(7) P=(V*V)/R kutokana na (3) na (5);

(8) P=(V*V*A)/(r*L) kutokana na (2) na (6).

Ambapo:
  • V=Volti/Voltage
  • I=Mkondo wa umeme/Current
  • R=Ukinzani/Resistance
  • P=Nishati ya joto inayozalishwa na umeme mkondoni/Dissipated Power
  • r=Kiini-ukinzani/Resisitivity
  • A=Eneo mkingamo katika waya wa umeme/cross-sectional area
Kimantiki, kuna mahitimisho mawili kutokana na formula hizi.

Mosi, kutokana na formula namba (6) ni wazi kwamba, kadiri umbali wa kusafirisha umeme unavyoongezeka nguvu yake inayopotea inaongezeka.

Yaani, “dissipated power is directly proportional to distance and current.”

Hii maana yake ni kwamba, ili tuweze kusafirisha “umeme wa mkondo-geu” kutoka bwawa la Nyerere au Mtera hadi Arusha bila kupotea sana, inabidi kujenga, sio vituo vya kupozea umeme wa mkondo-geu njiani (step-down transformer substations) kama Malisa anavyodai kimakosa, bali tunapaswa kujenga vituo vya kukuzia umeme huo wa mkondo-geu (step-up transformer substations).

Na pili, kutokana na formula namba (8) ni wazi kwamba, kadiri umbali wa kusafirisha umeme unavyoongezeka nguvu yake inayopotea inapungua.

Yaani, “dissipated power is directly proportional to voltage and inversely proportional to distance.”

FomuLa hii inahusiana na tekinolojia ya kusafirisha umeme wa mkondo-mnyoofu ambao hauna uhusiano wowote na transfoma-pozo wala transfoma-chocheo.

Tekinolojia hii inaitwA “High Voltage Direct Current (HVDC) Transmission Lines.”

Malisa hajaongelea kitu kuhusu mkono huu wa mjadala kwa makusudi, maana unafichua uzembe wa serikali katika suala zima la kupanga na kutekeleza miradi ya kuzalisha na kusambaza umeme.

Kwa vile tunapaswa kuachana na aibu ya kuhemea umeme Tanzania tunapaswa kuwekeza zaidi katika tekinolojia ya HVDC haraka iwezekanavyo, hata kama uamuzi huu unamaanisha kufunga mkanda.

Ukweli ni kwamba HDVC za masafa marefu zinaweza kupunguza upotevu wa umeme kwa sababu kadiri umbali unavyoongezeka upotevu wa umeme unapungua kwa mujibu wa fomula namba (8) hapo juu.

Kwa hiyo, uamuzi wa Tanzania kuhemea umeme kutoka ughaibuni ni Ushahidi kwamba Wizara ya Nishati haikutekeleza wajibu wake ipasavyo kwa wakati, na sasa inahaha kuokoa jahazi.

Na mpaka hapo hakuna "ufafanuzi wa ufafanuzi" utakaoweza kunibadilisha mawazo isipokuwa maelezo ya kwanini serikali ilipuuzia tekinolojia ya HDVC.

Na ninamwomba Malisa ajitokeze na kujibu pingamizi langu.
 
Tunakwepa vituo vya kupozea umeme et ni gharama kubwa karibu bi 20 zilitumika pale mateves arusha kili chotengenezwa kuanzia 2019 mpaka 2024,,, GHARAMA YA UMEME HUU WA ETHIOPIA tuna ingia nao mkataba ni wa sh ngapi..?? na sis TUTAPATA faida ya sh ngapi..?? na mikoa itakayo faidika ni mikoa ya kaskazin gharama za umeme kwa hii mikoa itakuwa tofauti na mikoa mingine?? mama anaupiga mwingi mi 5 TENAAAAA
 
Huyu dogo amekimbia Chadema ya Lisu na ameamua kuwa chawa wa mafisadi ya ccm
 
Upo vizuri mkuu akikujib nitag
 
Risk management basi , unapiga maths zako unaona ni wapi una incur losses kidogo basi unabeti hapo hapo.
 
waTanzania wanapenda kutwist mambo sana.
Umeme utauzwa Rwanda na Zambia kupitia vituo vya karibu na hizo nchi ila wanasahau kuwa Kanda ya Kaskazini pia wanaweza kuchukua 80MW +8MW za Tanga na Kilimanjaro, mbona hapa wanapiga chenga hawataki kukisemea?

Je Mwanzo na mwisho wa kusambaza umeme unaozalishwa kutoka Mwl Nyerere hydropower ni mikoa gani?

Serikali na wapambe wake hawana hoja ya kutofikisha umeme kwenye hiyo Kanda, wanataka kupiga tu pesa. Mbona huo Umeme ukisafirishwa kwa mfumo wa DC hakuna hizo loses wanazosema.
Yaani ununue umeme kutoka nje kupitis nchi nyingine wakati unayo ya ziada then unakuwa comfortable kabisa, siku mkikosana na serikali ya Kenya nchi inakuwa gizani ndipo mnaanza kumtafuta mchawi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…