Godlisten Malisa: Namuunga mkono Rais Magufuli kufungua vyuo vya elimu

Godlisten Malisa: Namuunga mkono Rais Magufuli kufungua vyuo vya elimu

Joined
Nov 27, 2019
Posts
35
Reaction score
146
Na GODLISTEN MALISA

Kwa maoni yangu nadhani hatua ya kufungua vyuo na taasisi nyingine ni muhimu japo ni muhimu zaidi kuendelea kuchukua tahadhari kama alivyosema Rais JPM. Ukweli ni kwamba janga la Covid19 sio jambo la muda mfupi kama ilivyotarajiwa kwamba litakuja na kupita. WHO wamesema it is here to stay. Kwahiyo hatutarajii maambukizi yataisha kesho au keshokutwa. Sasa tukisema tujifungie ndani tutajifungia hadi lini?

Kimsingi maisha lazima yaendelee japo kwa tahadhari. Hayawezi kuwa kama zamani lakini ni lazima yaendelee. Lockdown haiwezi kuwa suluhisho la kupambana na Covid19 kwa sasa. Hata nchi zilizofanya lockdown zimeanza kubadilisha mbinu. Lockdown ingeweza kuwa suluhisho kama ugonjwa ungekuwa wa mpito. Lakini kama utaendelea kuwepo, je tutajifungia ndani maisha yote?

Katika nchi zilizoendelea kama Marekani baadhi ya watu wameanza kulazimisha kutoka nje baada ya kuona kujifungia ndani pekee sio mbinu sahihi ya kupambana na janga hili. Madhara ya kujifungia ndani ni pamoja na uchumi "kuparalize". Leo njia nyingi za uchumi duniani zimedumaa kwa sababu ya lockdown. Tanzania japo maambukizi sio makubwa (pamoja na kwamba takwimu hazipo wazi) lakini ukweli ni kwamba athari za kiuchumi zinaweza kuwa kubwa kuliko athari za corona yenyewe.

Pamoja na kwamba hatujafanya lockdown lakini biashara nyingi zimeyumba, taasisi nyingi zimepunguza wafanyakazi, nyingine zimewapa watumishi wake likizo bila malipo. Mabenki nako hali ya kifedha sio nzuri kwa sababu mzunguko wa fedha mtaani umepungua kwa kiasi kikubwa. Wenye mikopo wanashindwa kurudisha kwa wakati kwa sababu vyanzo vyao vya fedha vimefubaa.

Mfanyabiashara mmoja wa madini mkoani Mbeya anmejiua kwa kujipiga risasi kichwani baada ya kushindwa kurejesha mkopo wake bank. Hapa Dar mmiliki mmoja wa shule alitaka kujiua kwa kujirusha ghorofani kwa sababu ya kushindwa kurejesha mkopo wake bank. Anasema watoto hawalipi ada kwa sababu hawaendi shuleni, lakini bank wanaendelea kumtaka apelee marejesho kila mwezi.

Kwa kifupi Covid19 imeleta taharuki nyingi, lakini nyingine hazikua za lazima. Just imegine "sociopolitical" conflicts zilizotokana na Covid19 ambazo hazikua na ulazima. Corona imesababisha Chadema kufurusha wabunge wake, Corona imesababisha baadhi ya viongozi katika wizara na idara nyeti za serikali kutimuliwa. Corona imesababisha mgongano usio wa lazima bungeni. Corona imesababisha mgogoro wa kidiplomasia na majirani zetu. Why all these??

Kwenye nchi zilizoendelea hali ni mbaya zaidi. Taasisi ya American Foundation for Suicide Prevention (AFSP) imerippoti kuwa "rate" ya watu wanaojiua imeongezeka zaidi kipindi huki cha janga la Corona kuliko ilivyokuwa awali. Taasisi hiyo imeeleza kuwa 25% hadi 30% ya wamarekani wanaojiua inahusishwa na visa vya Covid19. Kwa lugha rahisi ni kwamba katika kila watu wanne wanaojiua Marekani leo, basi mmoja amejiua kwa sababu zinazohusishwa na Corona. Too sad.!

Kwahiyo ukipima athari unaweza kuona umuhimu wa kuruhusu maisha yaendelee japo kwa tahadhari kuliko kuwafungia watu ndani. Kama kweli lockdown ingekuwa inasaidia basi nchi zilizofungia watu wake ndani maambukizi yangekuwa yamepungua kwa kiasi kikubwa. Lakini huko ndipo maambukizi yanaongezeka kwa kasi kila siku.

Kwahiyo ni muhimu kuruhusu maisha yaendelee japo kwa tahadhari. Vyuo vifunguliwe lakini wanafunzi wavae barakoa (ikiwezekana wagawiwe bure), wazingatie social distancing na kuepuka misongamano isiyo ya lazima, wanawe mikono kwa maji tiririka na sabuni.

Ofisi na taasisi zilizosimamisha shughuli zake nazo ziendelee na kazi japo kwa kuchukua tahadhari. Biashara zilizofungwa nazo ziendelee kwa kuchukua tahadhari. Kumbuka kwa mujibu wa WHO virusi vya Covid19 haviondoki leo wala kesho. It is here to stay. Kwahiyo ni muhimu kujifunza namna ya kuishi navyo badala ya kuvikwepa kwa kujifungia ndani. I stand to be corrected.!
 
Ni muhimu tukaendelea kuishi kwa tahadhari mpaka pale tiba halisi itapopatikana.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Yani mambo mengine ni upumbavu tu!
Hebu fikiria eti sasa watu waendelee kujifungia mpaka hadi marekani wagonjwa wafike 0 kutoka milion 1.6?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msemo wa ‘I stand to be corrected’ yanatumikaga na wengi isivyotakiwa.

Kusema ‘I stand to be corrected’ (maneno sahihi ni ‘I stand corrected’), ina maana kuwa baada ya kukosolewa, unakiri kuwa maoni yako au jambo ulilofanya halikuwa sahihi.
 
Mkuu Mwana wa Mtanzania uko sahihi, nimesoma huu uzi wako bado sijaona kwa kurekebisha.

This thing will be around for a quite long, cha msingi tahadhari lazima iendelee kuchukuliwa kikamilifu, lakini maisha hatuwezi kuyakimbia kamwe, lazima yaendelee.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli ni changer kwenye kila eneo.

Watanzania tunamhitaji kwa miaka 50 ijayo

Chadema wote say yeeeeiiiiyeeeee
 
Muhimu tuendelee kuchukua tahadhari binafsi,maisha yaendelee,wengine hali inazidi kuwa ngumu kwa sababu ya kujifungia ndani.
 
Mimi chuo naenda tena ikiwezekana mapema kabisa. Siasa pembeni, sijaona mtu akiugua wala kufa kisa corona. Hao mnaotangaza uko sijui walikuwa na matatizo gani mengine.

Corona ipo sana tutaishi nayo kwa muda mrefu. Hivyo vifo viko mtandaoni, mtaani sijaona hata mmoja kafa miezi yote hii. Next week naingia Kkoo kufanya manunuzi yangu ya muhimu.

Life goes on.
 
Msemo wa ‘I stand to be corrected’ yanatumikaga na wengi isivyotakiwa.

Kusema ‘I stand to be corrected’ (maneno sahihi ni ‘I stand corrected’), ina maana kuwa baada ya kukosolewa, unakiri kuwa maoni yako au jambo ulilofanya halikuwa sahihi.
Wewe ndio umekosea! I stand to be corrected maana yake ni kwamba niko tayari kukosolewa kwa haya niliyosema, ila mpaka sasa ninaamini huo ndio ukweli!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli ni changer kwenye kila eneo.

Watanzania tunamhitaji kwa miaka 50 ijayo

Chadema wote say yeeeeiiiiyeeeee

Huu ujinga wa kupenda kumsifia na kumtukuza Rais kwa kila jambo ndiyo unao sababisha mgawanyiko usio na tija ndani ya nchi yetu. Kila jambo, mtalitafutia kila aina ya sababu ili tu mligeuze na kuwa la kisiasa.
 
Wewe ndio umekosea! I stand to be corrected maana yake ni kwamba niko tayari kukosolewa kwa haya niliyosema, ila mpaka sasa ninaamini huo ndio ukweli!

Sent using Jamii Forums mobile app

Google ‘I stand to be corrected’ uone itakuletea nini. Huyo msemo ni kuwa waswahili mnachakachua msemo ulio sahihi wa ‘I stand corrected’ ambao maana yake nimeitoa.

Kama una nina ya kusema sina uhakika wa ninachokiongea, tumia maneno ya kawaida mfano:

I am not sure what the fk I’m talking about.

I have no clue what I just said.

Correct me if I am wrong, but....

I am stupid but I have an opinion....

Kuna njia nyingi unazoweza ku express doubt ya kile unachosema, ila epuka kusema ‘I stand to be corrected’. Ukisema hivi mtu ambaye ni native English speaker atadhani unakiri kukosea jambo ulilosema kabla. Najua utasema kuongeza maneno ‘to be’ inaashiria maana tofauti....pokea ushauri au acha.
 
Back
Top Bottom