Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Mwanaharakati wa haki za kijamii na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godlisten Malisa siku ya leo Jumapili Januari 12, 2025.amezungumza katika mkutano wa wanahabari uliofanyika mkoani Dar es Salaam
Malissa amezungumza mambo mengi kuhusu CHADEMA ikiwemo na uwepo wa wapambe ndani ya chama hicho akisema
"Tumekuwa na wapambe wa wagombea ambao wamekosa nidhamu kwa chama (CHADEMA) na wagombea ambao hawawaungi mkono, sasa kwa mujibu wa mwongozo wa taratibu za kuendesha uchaguzi ndani ya chama toleo la mwaka 2012 kifungu cha 2 (3) kinasema 'itakuwa ni marufuku kwa mgombea ama wapambe wake kusambaza taarifa zenye lengo la kukashifu mgombea au kiongozi wa chama'.
Ameongeza kwa kusema:
"Sasa pamoja na zuio hilo, tumeshuhudia uwepo wa maneno makali, ya kashfa, matusi ambayo yamekuwa yakitolewa kwa pande zote ambazo zinashiriki katika huu uchaguzi, na isivyo bahati ni kwamba yapo maneno ambayo mengine hayana staha yametumika kwa viongozi wetu na hapa sizungumzii upande mmoja"
"Tumeshuhudia baadhi ya watu wanajiita wanachama na ni wapambe wa wagombea wakitumia maneno kama fulani ni mropokaji, amehongwa, dalali, mbeba mikoba. Sasa hatuwezi kuwa na chama cha siasa watu wanatumia maneno na lugha zisizofaa katika kutafuta kura. Mimi binafsi siamini kuwa kudhalilisha upande mmoja kunakusaidia kupata kura za upande wa pili"
Source: Jambo TV, Habari Mpya