Godoro gani zuri kwa maana ya ubora?

Godoro gani zuri kwa maana ya ubora?

Tan foam

Qfl Dodoma

Anza na option ya kwanza ukikosa ndo ununue ya pili
 
Nahitaji kununua godoro la 5×6×10 naomba kufahamu kampuni gani ina magodoro imara na bora?
Budget yangu ni 280,000.
Tannfoam na arusha!

Kwa hela hiyo hakikisha lina density ya 28 chin ya hapo utaliwa hela! mengi yana density ya 23
waambie ya density ya 28
 
Yenye namba ndogo ya density ndo bora au namba kubwa ndo bora?
 
Density ni uwiano wa uzito na ujazo, kwa hayo magodoro mawili yenye ukubwa unaolingana lenye density kubwa litakuwa zito zaidi au gumu zaidi kwa maana litakuwa limeshindiliwa zaidi ko pia halitabonyea kirahisi hivyo hutoumia mgongo ukilalia.
Kweli elimu ni pana sana.

Waswahili wengi hatuangalii density,tunanunua tu.

Mkuu inawezekana godoro la inch 6 likawa na density nzuri kuliko godoro la inch 8 au 10 ?
 
Hiyo 28 Unit ni ipi? kg/m^3. au unit gani?
 
Back
Top Bottom