Godzila | King Zila Special thread

Akaliza

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2022
Posts
227
Reaction score
239
Wanajukwaa wa JF nawapa salam, ni matumaini yangu mnaendelea vizuri.

Japo ninayajua mambo machache kuhusu mtaalamu wa mziki wa aina ya HipHop- Godzila (King Zila) nimeona itakuwa bora kuwashirikisha nanyi mjazie mambo mnayoyafahamu kumhusu.

Sijawahi kuwa mfuatiliaji mzuri wa Mziki, na hii tabia si tu kwa nyimbo na wanamziki wa Tanzania ila hata muziki wa nje za nchi nao haukuwa katika vitu nilivyokuwa nikivipenda. Nakumbuka mwaka 2019 tukiwa darasani mwalimu wetu aliingia na kututaarifu kuhusu kuaga dunia kwa mwanamziki GODZILA. Baada ya kurejea nyumbani nikaingia mtandaoni na kuanza kuangazia nyimbo zake kadhaa, nilivyosikiliza wimbo wa STAY nilijikuta nimejawa na hisia kali mno (In a positive way), hapo nikaendelea kuangazia nyimbo nyingine nyingi.

Niliwahi kusikia habari chache sana kumhusu GODZILA, moja wapo ya stori nilizowahi kuzisikia ni kwamba aliandaliwa kuzimwa na the so called -Man in The black aliyekuwa akijinasibu kuisimamia Bongofleva na kuwainua vijana wengi licha ya kwamba mkulu huyo alitwishwa maneno yakuwa na tabia ya kikoloni. Bilinenga aliingia nakuwa replacement ya Godzila.

Kama una mengine unayoyajua kumhusu changia hapa ili tupate kumjua kiundani.

Quote kutoka kwa King Zila

" Rule number One, never complicate"
 
Godzilla hakuwa tishio kiasi cha kuandaliwa mtu wa kumzima. Japo alikuwa msanii mzuri hasa kwenye upande wa freestyle, ngoma zake nazozikubali zaidi ni 'salasala' na 'kingzilla' ft Makochali
 
Kuna freestyle aliipiga na Unju Bin Unuki wakiwa studio, beat ilikuwa ni ile ya STAY aliyeishuti hiyo video alikuwa ni Frederick Bundala (skywalker). Ukipata time ipitie huko U-Tube
 
Godzilla hakuwa tishio kiasi cha kuandaliwa mtu wa kumzima. Japo alikuwa msanii mzuri hasa kwenye upande wa freestyle, ngoma zake nazozikubali zaidi ni 'salasala' na 'kingzilla' ft Makochali
Hiyo salasala inatoka toka dah nasugua benchi flani mitaa ya Iringa nimpauka kinoma kila siku natembea kilometa kama 12 kwenda na kurudi.

Dah acheni tu.
 
Nadhan Godzzilla Ni moja ya wasanii waliokuwa na huwezo mzuri was kutumia Kingereza namkumbuka kwa Hilo tu
 
Bill Nas sio replacement ya Godzilla, na hata kaa afiti kwenye viatu vyake
 
Alikuwa na uwezo wa kukufanya utingishe kichwa kwa mizuka, but that's about it. Mistari haikuwa na maana wala tija. Pia alikuwa na ushamba wa kuchoresha.
 
Haya mambo yakuwa replaced uwa ni maneno ya kipuuzi tu.
Hivi wewe kama unamkubali msanii flani ana anatoa hits, unaweza eti shawishiwa umkubali mwingine na mtu?
Billnas alipoanza kutoka alihit kwa uwezo wake tu na kila mtu akamwelewa na chafu pozi yake. Mkmi billnas nilimwelewa sana na kuanza kumfuatilia ule wimbo alipmshirikisha TID na mpaka leo nauelewa.
Kila mwanamziki ana muda wa kuhit na kuisha, so kama una hit jiandae na maisha ya ku go down usije kufa kwa stress.
Muda ukipita umepita. Ndio maana uwa nacheka wanaosema wasanii wa zamani wanabaniwa, hakuna cha kubaniwa muda wao umepita. Ni sawa uwambie watoto wa juzi kuwa Mr nice alikuwa msanii mkubwa akipita nyomi linamfuata, uwa hafi nikirudi kusikiliza nyimbo zake nashangaa hata alikuwa anaimba nini.
Nikirudi kusikiliza nyimbo za Suma G nagundua ile michano na style haiwezi penya kwa kizazi hiki, same kwa juma nature.
Godzilla alikuwa anahisi anaishi US unyama mwingi na mziki baadae ukaanza mkataa akaanza jitengenezea mwenyewe nyimbo kwenye studio yake. Hits zake nyingi kazitengeneza Marco Chali, sijui aliamua jutegemea au waligombana hilo sijui.
Na ukumbuke kuwa waliomuibua Godzilla ni hao hao Mawingu nakumbuka kwenye hayo mashindano ya freestyle nadhani Dj fety ndie aliyekutana nao wakati akitafuta washindani. japo hakuwa mshindi wa kwanza lakini baada ya kuwa na Marco alipeea airtime kuliko hata Niki Mbishi.
 
Hii verse ya rule no one never complicate alisem kweny ngoma gan mkuu imenitoka kidg
 
Billnas alipoanza kutoka alihit kwa uwezo wake tu na kila mtu akamwelewa na chafu pozi yake
Jamaa namuonaga wakawaida sana.
Kila mwanamziki ana muda wa kuhit na kuisha, so kama una hit jiandae na maisha ya ku go down usije kufa kwa stress.
Muda ukipita umepita. Ndio maana uwa nacheka wanaosema wasanii wa zamani wanabaniwa, hakuna cha kubaniwa muda wao umepita
Moja Kati ya waamziki waliouweka mziki wa Tanzania kwenye ramani nzuri hasa upande wa Hip hop ni Juma nature Lakini Muda ukipita umepita Jamaa anajitahidi kurudi kwenye game lakini wapi the same kwa Saida karoli licha ya kujitahidi kurudi kwenye game baada ya zile ngoma za Diamond,Darasa na Belli 9 lakini akashindwa kutoboa.
 
Jamaa alikuwa ni kisanga
Kuna ile inaitwa"kila wakati" akiwa na g nacko alikuwa na kipaji.

Kiufupi tumepoteza vichwa vingi akiwemo zillah, langa kileo, ngwear nk
 
Unamfananishaje King na Bill nenga achana na moto wa King Zilla mpaka free style zake wasio kuwa zawa walipinda free style zake Billnas mweupe sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…