Akaliza
JF-Expert Member
- Apr 12, 2022
- 227
- 239
Wanajukwaa wa JF nawapa salam, ni matumaini yangu mnaendelea vizuri.
Japo ninayajua mambo machache kuhusu mtaalamu wa mziki wa aina ya HipHop- Godzila (King Zila) nimeona itakuwa bora kuwashirikisha nanyi mjazie mambo mnayoyafahamu kumhusu.
Sijawahi kuwa mfuatiliaji mzuri wa Mziki, na hii tabia si tu kwa nyimbo na wanamziki wa Tanzania ila hata muziki wa nje za nchi nao haukuwa katika vitu nilivyokuwa nikivipenda. Nakumbuka mwaka 2019 tukiwa darasani mwalimu wetu aliingia na kututaarifu kuhusu kuaga dunia kwa mwanamziki GODZILA. Baada ya kurejea nyumbani nikaingia mtandaoni na kuanza kuangazia nyimbo zake kadhaa, nilivyosikiliza wimbo wa STAY nilijikuta nimejawa na hisia kali mno (In a positive way), hapo nikaendelea kuangazia nyimbo nyingine nyingi.
Niliwahi kusikia habari chache sana kumhusu GODZILA, moja wapo ya stori nilizowahi kuzisikia ni kwamba aliandaliwa kuzimwa na the so called -Man in The black aliyekuwa akijinasibu kuisimamia Bongofleva na kuwainua vijana wengi licha ya kwamba mkulu huyo alitwishwa maneno yakuwa na tabia ya kikoloni. Bilinenga aliingia nakuwa replacement ya Godzila.
Kama una mengine unayoyajua kumhusu changia hapa ili tupate kumjua kiundani.
Quote kutoka kwa King Zila
" Rule number One, never complicate"