Ndiyo maana wazee wetu walisema ndoa ni msalaba, unabidi uubebe mpaka mwisho wa safari yako duniani, Mungu anakataa kuachana...
Nyamayetu sorry spelling Nyamayao!
Kuna tofauti sana kati ya mama na mzazi, mama anaweza kuwa hata Mbwa...lakini mzazi nitofauti...si kweli mama ndiye mlezi wa familia in all scenarios. Kama umeisha ona hii movie ya zamani kidogo inatwa When a Man Loves a Woman ilikuwa directed na Luis Mandoki na kuchezwa na Andy Garcia na Tina Majorino unaona yule mama alivyokuwa mlevi wa kutupwa hajali kabisa watoto! Hii ipo pia kwenye familia zetu nyingi kabisa unakuta mama ameamua kupigwa mikasi na kuwa mlevi ukigusia suala na kuachana wanakuwa wakali eti wao ni walezi wazuri kuliko kina baba thats I can not buy is crap idea. Kuna wazazi hulea watoto wa wenzao kuliko aliyewazaa bwana....kuna wamama (si wazazi) ni balaa hasa hufikia hata kufanyia vituko watoto wa kuwazaa wenyewe vituko kisa haelewani na baba yao....
Nakupa offa uje tuone hii picha kwangu off course na Belinda akiwepo maana huwezi jua....labda utaondokana na wazo eti wakina mama wanalea vizuri kuliko kina baba....
Masa
Mbu unavituko sana nilikuwa sijaona signature yako looohh haya mpwa!
Mzee kama ni mali nitamwachia kila kitu, ila watoto wangu aniachie...maana njemba nyingine ianze kubandua mama yao watoto watajisikia vibaya.....I will rather fight again to achieve mali zingine....
Mzee kama ni mali nitamwachia kila kitu, ila watoto wangu aniachie...maana njemba nyingine ianze kubandua mama yao watoto watajisikia vibaya.....I will rather fight again to achieve mali zingine....
na wewe ukioa mke mwingine hutambandua watoto wakisikia? huo ni ubinafsi
"Uchungu wa mwana, aujuae mzazi"Mtoto ni wa mama siku zote. Ndio maana watu wanapenda mama zao zaidi kuliko baba zao. Mwanamke anakimbilia kuchukua wanawe kwa kuwa ndio mwenye uchungu na watoto.
Nani kama mama.
Uchungu wa mwana, ajuaye mama.
duuuuuuuh, maaazee hiyo Avatar yako aha ahahaahaaaaaa π duuuuh! enhee, ngoja niangalie sinema ya bure kwanza, nitachangia hoja yako badae, duh!
Usiniambie tu kuwa bado unaangalia sinema na kusahau kuchangie hii hoja..Avatar ya Chamtuvima ni soo eeh!!
Endeleza hoja jukwaani utacheki picha baadae..
kuna shori aliwahi kuniambia sina mapenzi ya kweli......maana sina wivu,sijali akienda akirudi usiku wa manane poa tu.....akisema kachoka hataki mapenzi poa tu naenda viwanja......Kuna jamaa mkewe alipomtamkia "sikutaki, nataka talaka yangu," alichukua wanawe wawili na kujirusha nao toka juu ghorofani! Mwingine mahakama ilipoamuru akabidhi nyumba na watoto kwa mkewe, kwanza aliwaua wototo, kisha akaipiga kibiriti nyumba kabla yeye mwenyewe hajajiua! ....