Military Genius
JF-Expert Member
- Mar 3, 2019
- 761
- 1,464
Polisi wa mji wa Old Orchard, Chicago US waliinunua gari hii mwanzoni mwa miaka ya 1980 kabla ya baadae kumuuzia mwanaume mmoja kwa matumizi binafsi baada ya kuona wameanza kutoielewa gari hio, askari watatu walikufa kimaajabu ajabu baada tuu ya kuliendesha kwa siku kadhaa.
Inaelezwa kuwa jumla ya askari watatu waliowahi kuliendesha gari hili walijiuwa wenyewe baada ya kuzimaaliza familia zao kwanza, yaani kila askari alikuwa anaua familia yake yote, kisha na yeye anajiua.
Kati ya mwaka 1980 hadi 1990 viongozi wa makanisa mbalimbali walijitolea mara kadhaa kuliombea gari hili, ajabu ni kwamba wote walikua wanakufa kwa vifo vilivyotokana na ajali siku chache tuu baada ya kila mmoja kuliombea gari hili linaitwa Golden Eagle Car.
Hadi mwaka 2016 mmiliki wa gari hili alikuwa anaitwa Wendy Allen, lakini huyu naye alikiri kuwa gari hiyo haitumii mara kwa mara kwasabu ya mambo yasiyo ya kawaida anayokutana nayo, mara milango ya gari inajifungua yenyewe anapokuwa barabarani NK.
Taarifa zilisema kuwa Allen alikuwa hajapata madhara makubwa kama waliyoyapata watu wa nyuma waliowahi kuimiliki gari hiyo, na Hadi mwaka huo wa 2006 kulikuwa na vifo vya ajabu 32 vilivyotokana na gari hiyo japo idadi ilisemwa kuwa ilikuwa kubwa zaidi, vifo vya moja kwa moja vilikuwa 14.
Mwaka 2008 kuna mtoto mmoja aliigusa tuu gari hii, majuma machache baadae aliiua familia yake yote mpaka mbwa, akachoma moto nyumba na kisha kujiua na yeye. Gari hili pia limewahi kusababisha vifo vya watu 18 katika ajali iliyokuwa ndogo tuu.
Mwaka 2010 kundi la watu wa kanisa walienda kinyemela katika nyumba ya Allen na kulibondabonda gari hilo vipande vipande, wakavitupa sehemu tofauti tofauti, lakini siku chache baadae gari likakutwa liko barabarani, dereva akiwa ni Allen kama kawaida. Watu walianza kuhisi kuwa Allen ni mchawi japo yeye hukataa tuhuma hizo.
"Ninasema ni gari tuu limepitishwa katika maisha yangu, na watu wanaongea sana juu ya matukio yanayotokea kuhusiana na gari yangu, angalia familia yangu, tuko sawa, siyo? Kama gari linaua iweje familia yangu kila mmoja hafi.?
@military_Genius