Mie ni Yanga lia lia, nafurahishwa sana jinsi tunavyopiga boli la viwango vya Bundesliga.
Ukitoa Ihefu, hatuna timu ya kutushinda hapa bongo NBCPL sisi ndio wababe.
Ila sasa....... [emoji23]
Huko CAFCL hatujawahi kutoboa kabisa, hatujawahi fika hata robo fainali.
Nashangaaga wale wekundu wa msimbazi tuliowapiga bao 5 wapo vizuri sana kule CAFCL kuliko sisi, wananchi huwa tunakosea wapi jamani hadi tubaki wasindikizaji tu kule CAFCL?
Itabidi tujifunze kwa Simba japo ni mnyonge wetu huku NBCPL ila kule CAFCL wapo vizuri mno.
Daima mbele nyuma mwiko.